Na Denis Chambi, Tanga.
MASHIRIKA
yote yasiyokuwa ya kiserikali hapa nchini yametakiwa kuendelea kutekeleza wajibu
wao katika kulipa kodi kwa wakati sambamba na kusimamia sheria,
kanuni na taratibu zilizopo katika utendaji kazi kwa kuzingatia maslahi
ya taifa.
Wito huo
umetolewa na mwakilishi wa katibu tawala mkoa wa Tanga George Mbaga
wakati akifungua semina iliyoyakutanisha mashirikia binafisi yaliyopo
ndani ya mkoa huo ikiandaliwa na shirika la Foundation Civil Society
'FCS' kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kujiendesha , kuzingati sheria
miongozo na taratibu za nchi pamoja na kuwakumbusha wajibu wao katika
maendeleo ya Taifa hususan katika kutekelez kwa vitendo sheria ya
ulipaji kodi.
"Mashirika
yaliyo mengi yanasema ni mashirika ya huduma kwa hiyo hawana mamlaka ya
kulipa kodi lakini ukweli ni kwamba kila shirika limeajiri wa fanya
kazi hivyo ukishaajili ni lazima uende katika sehemu ya ulipaji kodi ni
muhimu kwa sababu maendeleo ya nchi yanategemea kodi hivyo ni lazima
wazingatie kuwa wanatekeleza kanuni na miongozo iliyotolewa na serikali"
alisema Mbaga
Aidha
alisema kuwa licha ya mashirika mengi yaliyopo hapa nchini kutegemea
fedha za wafadhili ili kuweza kujiendesha ni vyema kuzingatia sheria
kanuni na maslahi ya Taifa akiyataka kuwa na miradi ambayo inaweza
kuwasadia pamoja na kusimamia malengo yao waliyojiwekea.
"Mashirika
mengi yanategemea fedha za wafadhili, na unapotegemea wafadhili
pengine wanapenyeza ajenda ambazo sio sahihi kwa maendeleo ya na
utamaduni wetu hivyo wengi wakikosa wanakuwa hawatekelezi malengo yao
hivyo tunasisitiza taasisi hizi ziwe na miradi endelevu, ziwe na
maengo ya kati na ya muda mfupi ambayo yanatekelezeka " alisisitiza.
Pamoja
na hayo Mbaga aliyapongeza mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo
kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakiunga mkono jitihada za serikali za kupiga
vita vitendo vya ukatili wa kijinsia vilivyokuwa vikokea katika jamii
ambako wamekuwa wakitoa huduma kwa karibu zaidi.
"Kulingana
na taarifa za utendaji wa zilizowasilishwa kwa msajili wa mashirika
kwa kipindi cha 2022/2023 mashirika yamechangia kwa kiwango kikubwa
maendeleo hasa katika utekelezaji wa afua za afya, elimu ukatili wa
kijinsia, msaada wa kisheria uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na
kutoa huduma stahiki kwa makundi maalum wakiwemo wenye ulemavu, wazee
, wajane na wanao ishi kwenye mazingira hatarishi" aliongeza Mbaga.
Akizungumza
kwa niaba ya shirika la Foundation For Civil Society Nicholaus
Mhozya ambaye ni afisa Program mwandamizi alisema kuwa licha ya juhudi
mbalimbali wanazoendelea kuzifanya katika kuisaidia serikali ni vyema
wakatambua kuwa wana wajibu mkubwa wa kuendelea kulipa kodi kwa kufuata
sheria kanuni na taratibu zinazowaongoza ili kuepuka adhabu ambazo
wanaweza kukumbana nazo ikiwa ni pamoja na kufutiwa usajili.
"Kwa
nadharia tu ya kawaida ni kwamba sisi ni mashirika ambayo sio ya
kiserikali hatutengenezi faida za kugawana, na hata inapotokea
tunategeneza faida ni zile ambazo zinarudi kwenye jamii wengine
tumekuwa tukijisahau kwamba kwa sababu tu hatutengenezi faida kwahiyo
hatutakiwi kulipa kodi kumbe sii hivyo inapokuwa ishakuwa tasisi na
inajiendesha kisheria kuna mazingira ambayo yatakulazimu ulipe kodi"
"Kulipa
kodi ni wajibu wa kuweza kuleta maendeleo lakini kuepukana na migogoro
ambayo mwisho wa siku unaweza kuingia kwenye adhabu ambayo itakukatisha
tamaa kufanya kazi za jamii" alisema Mkondya.
Mkondya
alisema mashirika mengi yamekuwa yakishindwa kusimamia malengo yao
waliyojiwekea na kukiuka sheria na taratibu zinazowaongoza hapa nchini
hivyo kujikuta wanakiuka taratibu za nchi ambapo mpaka sasa mashirika
yapatayo elfu nne yameshafungiwa
"Tunafahamu
kuwa katika hii sekta tunafanya kazi na watu wa aina tofauti na
kuanzisha taasisi ni suala la hiari, serikali inatambua kwamba tuna
mchango kwenye jamii katika kusukuma maendeleo lakini katika michango
yetu haitupi ruhusa ya kujiendesha bila kuzingatia sheria zilizopo ni
vyema kuendelea kuzingati na kutekeleza kaa vitendo ili malengo
waliyojiwekea yaweze kutimia, "
Shirika
hilo la Foundatio For Ciliv Society (FCS) lililoanzishwa mwaka 2002
limekuwa ni mwamvuli kwa mashiriki na taasisi mbalimbali zisizokuwa za
kiserikali hapa nchini ambapo limekuwa likifanya kazi kwa karibu katika
kuyawezesha ruzuku pamoja na kuyajengea uwezo wa kujiendesha hasa
kupitia sheria inayowasimia na kuwaongoza hapa nchini.
Akizungumza
mwakilishi baraza la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwa mkoa wa
Tanga Miraji Malinda amesema kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa
fedha ndani ya mashirika mengi kwaajili kujiendesha akiwaomba viongozi
kuongeza wigo wa ushirikiano baina yao na wadau wengine pamoja na
serikali.
"Changamoto ya
upatikanaji wa maswala ya fedha umekuwa ni mkubwa kwa upande wa
mashirika lakini tuone ni namna gani ya kuweza kuongeza wigo wa
kuaminika kwa wafadhili kuongeza ushirikino na serikali pamoja na wadau
mbalimbali" alisema
"Tunaiomba
serikali kuweza kutuunganisha na wadau wengine mfano kupita mashirika
ya kibiashara hasa kayika mpango mkakati wa uendelevu wa Cooperate
Social Responsibility 'CSR' ambayo inatakiwa ije kwetu sisi mashirika
ambayo ndio tunafanya kazi kwa karibu sana na jamii" alisema Malinda.
Foundation
Civil for Society limekuwa likijengea uwezo mashirika yote yasiyokuwa
ya kiserikali ambapo hadi sasa limefika katika mikoa kumi ya Tanzania
bara wakilenga pia kuifikia mikoa yote nchini kwa lengo la kuhakikisha
ustawi ndani ya mashirika hayo unakuwepo ambayo yatachangia katika
maendeleo ya Taifa.
Mwakilishi wa baraza la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwa mkoa wa
Tanga Miraji Malinda.
Post A Comment: