Na John Walter-Manyara

Na John Walter-Manyara
Kufuatia kuanza ugawaji mahindi ya msaada wilayani Babati mkoani Manyara  ili kupunguza makali ya njaa kutokana na upungufu wa chakula kwa wananchi uliosababishwa ukame, mfanyabiashara mmoja  mkoani hapa, anadaiwa kushikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na mifuko 42 yenye ujazo wa  kilo hamsini kwa kila mfuko.

Hayo yamesemwa na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kata ya Maisaka  ambapo wamesema taarifa hizo walizipata kutoka kwa raia wema ambapo baada ya kufuatilia wakiwa na polisi walikuta mahindi hayo kwenye nyumba ya mwananchi mmoja  eneo la Changarawe majira ya saamoja Usiku Machi 4,2023.

Katibu wa CCM kata ya Maisaka Apolonary Hhayuma amesema licha ya Serikali kutoa msaada wa Mahindi hayo wapo baadhi ya wananchi katika kata hiyo wanalalamika kukosa.

Hata hivyo walipomhoji mwananchi huyo alisema ni mzigo wa tajiri mmoja Babati ambapo walimtafuta na alipofika akakana kuwa hausiki na mzigo huo na kwamba yeye ni mfanyabiashara.

Amesema kuwa, baada ya kukamata mahindi hayo wakishirikiana na jeshi la Polisi waliupeleka mzigo huo hadi kituo cha Polisi Babati na mtuhumiwa.

Mahindi hayo  ya bei nafuu ambayo kilo huuzwa kati ya 800, yametolewa na Wakala wa Hifadhi ya Taifa Chakula (NFRA) ili kukabiliana na uhaba wa chakula.
Share To:

Post A Comment: