Na Immanuel Msumba ; Longido
Mazingira safi ni kitovu cha afya bora na maendeleo kwa wananchi. Ili kufikia lengo la kuwa na mazingira safi, ni lazima kuwa na mikakati endelevu ya kudhibiti uchafuzi wa makazi kutokana na taka zinazozalishwa kila siku.
Ili kuweka usimamizi endelevu wa usafi katika makazi ni lazima kuweka misingi ya usimamizi, tathmini na kuchukua tahadhari kuhusu madhara kwa mazingira, kwa kudhibiti taka kuanzia zinapozalishwa, ukusanyaji, usafirishaji na utupwaji wake.
Mikakati ya usimamizi wa taka inapaswa kuzingatia kanuni za "3R" ambazo ni kupunguza, kurejesha na kuchakata taka. Hii inamaanisha kuwa ni muhimu kupunguza idadi ya taka zinazozalishwa, kwa mfano, kwa kudhibiti matumizi ya plastiki, kurejesha taka kwa njia ya kuchakata na kutumia tena kwa ajili ya uzalishaji, na kuchakata taka ambazo haziwezi kurejeshwa kwa matumizi mengine.
Hali ni tofauti katika Wilaya ya Longido Mkoani Arusha ambapo wananchi wapo hatarini kupatwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na dampo na bwawa la maji taka kuwepo katikati ya makazi ya watu bila uzio ndani ya vijiji viwili ya Kimokowa na Endoreke katika Kata ya Kimokowa.
Asilimia 98 wananchi wake wanategemea ufugaji ambapo mifugo mingi ikiwemo wanyama pori kama zile swala,twiga na digidigi hujikuta wakiwa katikati ya dampo hilo wakila taka na wengine wakinywa maji taka yanayozalishwa katika makazi ya wananchi hao sambamba na watoto wanaopeleka mifugo malishoni kuwapitisha katika maeneo ya dampo ilo ambapo ni hatari kiafya.
Solomoni Kool ni Diwani wa Kata ya Kimokowa ambapo anatueleza kuwa walianzisha dampo hilo katika kata hiyo ambalo linazungukwa na Vijiji viwili ambapo walitenga eneo hilo kwa ajili ya dampo la taka ngumu na maji taka.
"Tulitenga eneo hili kwa ajili ya kusaidia wananchi wa mji wa longido na Namanga kuweza kuwa na eneo maalum ya kutupa takataka zinazozalishwa ndani ya jamii yetu lakini hali imekuwa tofauti kwanimifugo wanaokota takataka hizo hususani salifeti na kuzitafuna,pia eneo hili ni la ukame sana wanatumia maji yale kunywa jambo ambalo limekuwa changamoto kubwa sana kwa jamii ya kifugaji."
"Kupitia baraza la madiwani tumetenga bajeti kwa ajili ya kuweka uzio katika eneo lote linalozunguka dampo lile,lakini tunaendelea kusisitiza na kuwaomba wadau wa maendeleo wilayani hapa kushirikiana na halmashauri kuweka uzio pale ambapo halmashauri itaishia ili kunusuru hali mbaya inayoendelea katika jamii ile ya wafugaji wanaozunguka eneo lile." Aliongezea solomon
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Namanga Hassan Ngoma amesema kuwa kwa sasa huduma ya dampo la kimokowa hawalitumii kutokana na kushindwa kumlipa mkandarasi ila sasa wanahangaika wenyewe kama wananchi baada ya kujaza takataka majumbani huwa wanatumia bodaboda na pikipiki za matairi matatu {Virikuu} kwenda kutupa takataka katika mto ambao unatiririsha maji kwenye vijiji ya jirani vya jamii ya kifugaji.
"Kwa sasa wananchi wa Namanga wanamwaga takataka darajani hapo karibu nakatoliki,muda huu hatuna gharama rasmi mtu anajaza takataka zake analipia elfu 1000 usafiri uanshushiwa hapo mtoni maisha yanaenda,ila kwa upande wa maji taka bwana afya anafanya mpango kwa watu wote wanaotaka kuvutiwa kisha anaagiza gari kutoka Arusha ndipo linavuta linapeleka kule kwenye dampo la kimokowa"
"Sisi kama Kata tulishafunga kumwaga takataka pale darajani kwani hapa tunakituo kikubwa cha forodha {one stop border} kinazalisha uchafu mwingi ndio maana tulilazimika kutafuta mkandarasi ili takataka hizi ziwe zinatupwa kule kimokowa kwenye lile eneo ambalo lilitengwa"
"Athari zipo nyingi sana pale pembeni kuna mto tunapomwaga takataka hizi na maji ya mvua yanapotiririka pale yanakwenda kwenye jamii ya wafugaji ambapo kule kuna mifugo ambapo ukienda uchafu kule ngombe watakunywa na wakishakamuliwa maziwa yataletwa kwetu ndipo tutakunywa uchafu na kupata magonjwa ya mlipuko."
"Tumeshwindana na mkandarasi kutokana na gharama za uendeshaji kwani mapato hayakuwa mazuri sana hivyo tunaiomba Halmashauri kuangalia namna bora kusaidia mji huu wa Namanga" Aliongeza
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya hiyo Marco Henry Ng'umbi ameeleza kwamba lile eneo lipo wazi pembezoni kuna vijiji vinalizunguka na watoto wa shule wanapita pale na panakila aina ya uchafu ni hatari kwa maisha ya watoto wetu,Pia eneo lile ni la wafugaji mifugo inapita kula uchafu na uchafu kwa mifugo haufai hususani ni mapitio ya wanyama pori eneo lile wanyama kama twiga,tembo,swala wakila uchafu huu na kunywa maji yale itakuwa changamoto"
"Pale lazima tuokoe maisha ya watu,mifugo na wanyama pori wetu natuendelee kuhifadhi na kutunza mazingira ili kuacha takataka kusambaa na kwenda maeneo tofauti"
Kwa kuongezea, ni muhimu kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kudumisha usafi katika makazi yao, na pia kutoa mafunzo juu ya jinsi ya kudhibiti taka zao kwa njia salama na endelevu. Hii inaweza kufanywa kwa kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira na athari za uchafuzi wa mazingira kwa afya ya binadamu na viumbe hai wengine.
Mikakati ya usimamizi wa taka inapaswa kuzingatia kanuni za "3R" ambazo ni kupunguza, kurejesha na kuchakata taka. Hii inamaanisha kuwa ni muhimu kupunguza idadi ya taka zinazozalishwa, kwa mfano, kwa kudhibiti matumizi ya plastiki, kurejesha taka kwa njia ya kuchakata na kutumia tena kwa ajili ya uzalishaji, na kuchakata taka ambazo haziwezi kurejeshwa kwa matumizi mengine.
Kwa kuzingatia mikakati ya usimamizi wa taka, inawezekana kupunguza athari za uchafuzi wa mazingira kutokana na taka. Athari hizi zinaweza kujumuisha kuharibu ardhi na maji, kuchafua hewa, kuathiri afya ya binadamu, na kuathiri viumbe hai wengine. Kwa hiyo, ni muhimu kuendelea kuboresha mikakati ya usimamizi wa taka ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira na kuhakikisha mazingira safi kwa ajili ya maendeleo endelevu ya jamii na taifa kwa ujumla.
Post A Comment: