Na Denis Chambi, Tanga.
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA kanda ya Kaskazini Godbless Lema ameendelea kusimamia kauli yake
aliyoitoa hivi karibuni kuwa shughuli ya madereva waendesha pikipiki
maarufu kama Boda boda sio kazi badala yake inauwa nguvu kazi ya Taifa
la kesho akisistiza kuwa bado kundi hilo ni janga lililopo hapa nchini
wengi wakishindwa kuyamudu maisha wanayoishi na familiya zao.
Lema
ameendelea kusisitiza kauli hiyo akiwa mkoani Tanga march 20 , 2023
katika mkutano wa hadhara ikikumbukwa kuwa mara tu alipowasili hapa
nchini january 2023 akitokea Canada alikokuwa tangu mwaka 2020,
ambapo mara baada ya kukutana na mamia ya wafuasi wa chama hicho mkoani
Arusha aliizungumza na hatimaye kuibua baadhi ya viongozi wa vyama vya
siasa pamoja na uongozi wa Bodaboda wakimtaka akanushe kauli yake na
kutokuibize kazi hiyo lakini bado ameonyesha msimamo wake.
"Nasema
sifuti kauli na leo tena napigilia msumari kuwa udereva boda boda sio
kazi ya maana na watu wanazidi kuwa masikini na hii inajenga ufukara,
bodaboda zimeongeza vilema na wajane leo hii kuna watu
wanapoteza ndugu zao na maisha kwa sababu ya ajali za boda boda , "
alisema Lema
Aidha
Lema ameeleza kuwa kuna athari ambazo zinaweza kujitokeza hapo baadaye
kutokana na wazazi walezi na jamii kwa ujumla kushindwa kuwalea watoto
katika maadili mema jambo ambalo linaweza kuchoche kushamiri kwa vitendo
vya ukatili sambamba na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
"
Watoto wengi wanaozaliwa sasa hivi hawalelewi na wazazi wao ipasavyo
kama nyakati za wazee wetu je! Hivi meangalia taifa hili baada ya miaka
30 nchi itakuwaje nyie? ndio maana sasa hivi tunashangaa kuna tabia
zinazuka umasikini umekuwa mkali kuwanyima nafasi kwa wazazi
kuwaangalia watoto" aliongeza Lema.
Awali
akizungumza mjumbe wa halmashauri kuu ya CHADEMA Taifa Grace Kiwelu
alimpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa hatua aliyochukuwa ya
kufungua milango na kuridhia mashirikiano baina ya vyama vyote vya
siasa pamoja na kuruhusu mikutano ya kisiasa akisema kuwa licha ya hayo
yote bado CHADEMA itaendelea kusimamia msimamo wake kuhubiri umuhimu wa
kupatikana kwa katiba mpya.
"Niwashukuru
sana viongozi wetu wa vyama viwili wa Kitaifa wa Chama Cha Mapinduzi
'CCM' na Chama cha Demokrasia na Maendeleo 'CHADEMA' kwa kuleta
maridhiano leo watanzania tunazungumza , tumekuwa kwenye lifungo cha
miaka saba bila watanzania kuzungumza"
Mkutano
huo uliofanyika katika viwanja vya kata ya Msambweni ulihudhuriwa pia
na aliyewahi kuwa Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi
'MNEC'.
Pamoja na
hayo chama hicho kimtembulisha uongozi mpya wa CHADEMA ngazi ya wilaya
ukiongozwa na Rashid Jumbe ikikumbukwa kuwa katika ziara ya mwenyekiti
taifa Freeman Mbowe aliyoifanya hivi karibuni mkoani Tanga aliuvua
madaraka uongozi uliopo na kuwachagua wengine hii ikilenga hasa kuzidi
kukiimarisha chama hicho kuanzia ngazi za chini.
Uongozi
huo mpya unaoongozwa na aliyekuwa mwanachama wa ACT Wazalendo na ambaye
baadaye kuhamia CHADEMA kwa sasa akikaimu nafasi ya mwenyekiti , Khalid
Hamza kaimu katibu, Shaban Ngozi aliyeteuliwa kuwa katibu mwenezi wa
chama hicho, Zima Mohammed akikaimu nafaai ya baraza la wazee, Zena
Khamis kaimu mwenyekiti Bawacha, Amos Chiluda Mwenyekiti wa wazee
Selestin Kiria mweka hazina wa jimbo na wengine wengi waluokaimu nafasi
zilizoachwa wazi mara baada ya mabadiliko kitoka uongozi uliopita.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Grace Kiwelu akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CHADEMA (kushoto) mkoa wa Tanga akisalimiana na aliyewahi kuwa MNECwa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Tanga ambaye walimualika katika mkutano huo.
Uongozi mpya wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Tanga uliotambulishwa rasmi katika mkutano wa hadhara wa mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Kaskazini Godbless Lema uliofanyika mkoani Tanga March 20,2023.
Post A Comment: