Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil T. Abdallah amefanya uzinduzi rasmi wa Baraza la 32 la Wafanyakazi wa Wakala wa Vipimo lililofanyika kwenyeUkumbi wa NSSF ilala, Dar es Salaam.
Akifungua Baraza hilo Dkt. Hashil amemshukuru Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia SuluhuHassan kwa maelekezo na miongozo yake ambayo inaisaidiaWizara na taasisi zake kutekeleza mipango na mikakati yakukuza uwekezaji, ufanyaji biashara, uendelezaji wa viwanda nakuboresha mazingira kwa ujumla wake ya ufanyaji Biasharakatika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kadhalika, amewapongeza wajumbe wa baraza la wafanyakazikwa kuaminiwa na kuchaguliwa kuwa wakilisha watumishiwengine kwani uteuzi wao wa kuingia kwenye baraza la Wafanyakazi umezingatia sifa zao kwenye utendaji pamoja nauwajibikaji ndani ya taasisi.
Dkt. Hashil pia, ameupongeza sana uongozi wa Wakala waVipimo kwa jinsi unavyo ongoza taasisi hii na kwa uongozimahiri wa Mtendaji Mkuu pamoja na Jumuiya ya Wafanyakazikwa ujumla na kwa kuona umuhimu wake kushiriki katikaufunguzi wa baraza jipya la Wafanyakazi.
Ameeleza kuwa maendeleo ya taasisi ya WMA yanaonekanakatika kutekeleza majukumu yake ya msingi ya Kisheria ikiwana jukumu kuu la kumlinda mlaji kupitia matumizi sahihi yavipimo na hayo ni mafanikio ambayo yanaonekana wazi hasakatika siku za hivi karibuni ambapo Wakala imeanza kutoahuduma mpya za kuhakiki dira za maji na mita za umememaeneo ambayo yalikuwa yakilalamikiwa kwa kiasi kikubwa naWananchi kwa kulipa gharama kubwa kuliko kiasi cha hudumawanayopata.
Aidha, Dkt. Hashil amewahamasisha Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kuunganisha nguvu zao kwa kufanya kazi kwabidii, juhudi na maarifa ili kwa vitendo kuunga mkono juhudi zaSerikali ya awamu ya sita kwa kutoa huduma bora na kupunguzakero na malalamiko ya Wananchi dhidi ya Serikali.
Vilevile Dkt. Hashil, amewaasa wajumbe wapya wa barazakutumia nafasi vizuri kufanya tathmini ya kina ya jinsiwalivyotekeleza majukumu yao ya kibajeti na kiufanisi katikamwaka uliopita na namna wanavyoweza kujipanga katikavipaumbele vya taasisi kwa mwaka ujao wa fedha ili kutimizamalengo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vilevile, amewataka wajumbe kuongeza juhudi katika kufanyakazi na kuondokana na kufanya kazi kwa mazoea.
Post A Comment: