Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, akiwa ameshika keki maalumu aliyoandaliwa na Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa watu wenye Ulemavu Sabasaba-Singida wakati wa ziara yake mkoani hapa ya kukagua shughuli mbalimbali zilizo chini ya wizara yake.
Na Dotto Mwaibale, Singida
NAIBU Waziri,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi,
amezitaka Halmashauri za Wilaya na Manispaa nchini kuacha urasimu wa kutoa
fedha zilizotolewa kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu
zinazotokana na asilimia 10 ya mapato ya halmashauri hizo.
Katambi alitoa maagizo hayo juzi katika ziara ya kukagua miradi
inayotekelezwa inayotokana na asilimia 10 za mapato ya halmashauri wakati
akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani hapa.
Hatua ya Katambi kutoa maagizo hayo ilifuatia baada ya Mwenyekiti
wa Kikundi cha Vijana Chapa Kazi, Mwanahamisi Omari, kulalanikia kucheleweshewa
kupatiwa fedha za kulipia tripu 50 za mchanga wanaotumia kufyatua matofali
baada ya halmashauri hiyo kuwapa mkopo wa Sh. Milioni 25.
“ Mheshimiwa Naibu Waziri tunachangamoto kubwa ambayo
inatukwamisha na kushindwa kuendelea na ufyatuaji wa matofali fedha yetu
tuliopewa awali imekwisha sasa ni siku ya tatu kila tukienda pale halmashauri
tunapigwa danadana hasa pale ofisi ya Maendeleo ya Jamii mara tunaambiwa hela
hizo zitatolewa mpaka mhandisi aje kwenye mradi kuhakikisha kama mchanga huo
upo, mara tumsubiri mkurugenzi jambo ambalo linatuchelewesha,” alisema Omari.
Katambi baada ya kupokea malalamiko hayo akazitaka halmashauri
zote kuacha kufanya urasimu huo ukizingatia kuwa fedha hizo zinatolewa na
halmashauri kwa lengo la kuyasaidia makundi hayo na unapojitokeza urasimu huo unarudisha
nyuma maendeleo ya walengwa hao.
Aidha, Katambi aliagiza taasisi zote za Serikali zinapotekeleza
miradi ikiwemo ya maji na ujenzi wa madarasa na miundombinu mbalimbali itoe
kazi hizo kwa kununua matofali, vifaa vya chuma na vifaa vingine kutoka katika vikundi hivyo
ili vikuze mitaji yao.
Katambi alisema taasisi hizo zinapofanya sherehe zao hasa katika
mikoa ambayo ina vyuo vya ufundi ziwe zinakwenda kununua keki, upambaji na sare
zinazotengezwa na wanafunzi wa vyuo hivyo zikiwemo za Chama Cha Mapinduzi (CCM)
pamoja na bendera ya Taifa ili kuviinua kiuchumi badala ya kwenda kuagiza nje.
Aliwaomba wataalamu waliopo inapotekelezwa miradi hiyo kujenga
tabia ya kuvitembelea vikundi hivyo na kutoa elimu ya namna ya matumizi ya
fedha hizo jambo litakalosaidia kupata bidhaa bora zinazozalishwa pamoja na
kuondoa matumizi mabaya ya fedha zilizotolewa kwenye vikundi.
Akizungumzia kukua kiuchumi kwa vyuo hivyo, aliwataka walengwa
hao kuondoa dhana ya kuwa wajasiriamali badala yake wawe wafanyabiashara wa
kati na hata kufikia hatua ya kufungua makampuni yao makubwa kutokana na kazi
zao wanazo zifanya na kuziomba halmashauri kutoa maeneo kwa bei nafuu kwa
makundi hayo ili wajenge ofisi zao na kufungua viwanda.
Katambi pia aliziagiza halamashauri kuviongezea vikundi
vinavyofanya vizuri kurejesha mikopo inayokopeshwa akikitolea mafano kikundi
cha vijana cha St.Vidicon Manyoni Computer Workshop ambacho kilianzishwa Julai
2020 chini ya umoja wa mafundi wenye ujuzi wa fani mbalimbali waliokubaliana
kufanya kazi kwa kushirikiana.
Aliongeza kuwa wanafunzi wanaopata fursa ya mafunzo ya miezi
mitatu yanayowezeshwa bure na Ofisi ya Waziri Mkuu wanapomaliza mafunzo yao
halmashauri iwe inawapa mikopo kwa ajili ya kufungua viwanda vidogo vidogo
badala ya kukaa mitaani na ujuzi wao.
Katika ziara hiyo Katambi alitembelea miradi ya vijana hao katika wilaya za Manyoni, Ikungi, Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa watu wenye Ulemavu Sabasaba kilichopo Manispaa ya Singida, Shamba Kitalu Nyumba lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida Ilongero na kukagua ujenzi wa ukumbi wa CCM unaojengwa wilayani Manyoni.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, akimlisha keki mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, akisalimiana na Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani mara alipowasili wilayani Manyoni kuanza ziara yake hiyo juzi mkoani hapa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, akikagua ujenzi wa ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni.
Ukaguzi wa ukumbi huo ukiendelea. Kushoto ni Mjumbe wa Halimashauri Kuu CCM Wilaya ya Manyoni, Mjumbe wa Baraza UVCCM Mkoa wa Singida na Mjumbe wa Kamati ya Ujenzi wa Ukumbi wa CCM Wilaya ya Manyoni, Ngwigula Shigela.
Afisa Maendeleo ya Jamii, Wilaya ya Manyoni, Flavia Kiwango (kulia) akisoma taarifa ya miradi ya maendeleo ya Vijana wilayani humo mbele ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi (kushoto), Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Elias Mollel na wa pili kulia ni Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani.
Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha St.Vidicon Manyoni Computer Workshop, Fidel Timoth (kulia) akisoma taarifa ya kikundi hicho kwa Naibu Waziri Katambi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, akikagua vifaa vinavyotengenezwa kwa chuma na kikundi cha vijana cha St.Vidicon Manyoni Computer Workshop,
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, akiwa amekaa na msafara wake na maofisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Singida kwenye sofa zilizotengenezwa na kikundi cha Vijana cha St.Vidicon Manyoni Computer Workshop wakati wa ukaguzi wa shughuli za vijana waliopata mkopo kutoka halmashauri.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, akielekeza jambo baada ya kuangalia majiko yaliyotekenezwa na vijana wa kikundi cha St.Vidicon Manyoni.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, akisalimiana na mmoja wa WanaKikundi cha Vijana cha Chapakazi cha Wilaya ya Ikungi, Ashura Abubakari baada ya kuwasili wilayani hapo juzi katika ziara yake hiyo ya kikazi.
Vijana wa Kikundi cha Chapa Kazi cha Ikungi, wakinyoosha mikono mbele ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha nyingi kwa ajili ya kuendesha miradiya maendeleo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, akikagua matofali yanayofyatuliwa na Vijana wa Kikundi cha Chapakazi cha Wilaya ya Ikungi. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Mwanahamisi Omari. Na kushoto ni Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi katika shughuli hiyo, Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Dijovson Ntangeki.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi (kulia) akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Ikungi na Vijana wa Kikundi cha Chapakazi wakati akikagua Shamba la Kitalu Nyumba lililopo nje ya Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Richard Rwehumbiza
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu cha Sabasaba, Fatuma Malenga baada ya kufika chuoni hapo wakati wa ziara yake hiyo ya kikazi. Katikati ni Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Singida, Ally Mwendo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, akizungumza na mwanafunzi wa fani ya ushonaji nguo wa chuo hicho.Janeth Lucas.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, akiangalia nguo za CCM zilizoshonwa na wanafunzi wa chuo hicho.
Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani, akimlisha keki mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho wakati wa ziara ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi,
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, akizungumza na Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana na Wanagenzi cha Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ilongero, Frida Dastan, baada ya kutembelea Shamba Kitatu cha zao la nyanya zinazilimwa na vijana hao baada ya kupatiwa mkopo wa Sh.Milioni 10.
Post A Comment: