Na; Elizabeth Paulo, Dodoma
Vijana nchini wametakiwa kusemea maendeleo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi imara wa Mheshimiwa Samia Suluh Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuvunja taswira ya miaka kadhaa ya nyuma la kuwachukulia vijana kama kundi la kuchochea mabaya.
Mstahiki meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe Ameeleza hayo wakati wa Uzinduzi wa Jamii Mpya mkoa wa Dodoma yaliyoambanana na Bonanza la michezo mbalimbali na wasanii katika viwanja vya Shule ya Dodoma secondary.
Amesema upya wa jamii hiyo ni pale ambapo vijana wanapata nguvu mpya na kutambua, kukiri na Kuishi kauli mbiu ya Jamii Mpya "Mama yangu Nchi yangu Kazi iendelee"
Upya wa jamii hii ni pale ambapo tutakiri kwamba Tanzania ndiyo Nchi yetu na lazima tuipende Sisi vijana tusiwe kama waajiriwa wa Wizara ambao wanaweza kuhama Kutoka wizara moja au nyingine, Huwezi ukawa mtanzania ukahama nchi bado ukaita ile ni nchi yako. Amesema Mwamfupe
Amewaasa vijana kujiamini na kujikita katika maridhiano hivyo kujikita katika harakati za kupata maridhiano kati ya kizazi kimoja na kingine kwani mara nyingi kuna kuwa na ufa au tofauti ya fikra Kati ya kizazi kimoja na kingine.
Tuwe mfano wa kuingwa kwamba Sisi tuongoze maridhiano katika jamani bila kujali tofauti za itikadi za kisiasa,Dini na hata hali ya mtu yeyote lakini Vijana tunapaswa kuwa viongozi wa maridhiano?ambayo Mheshimiwa Rais anayasisitiza sana. Amesisitiza Mwamfupe
Aidha amewatakia michezo mema timu ambazo zinashiriki michezo hiyo kucheza kwa kupendana kwani ushindani siyo uadui.
Kwa upande wake Mwamvua Somji Katibu wa Jamii Mpya Kanda ya Kati inayojumuisha Singida na Dodoma Amesema Jamii Mpya ni Taasisi iliyoanzishwa inayoenda sambamba na kampeni ya MAMA YANGU NCHI YANGU kwa lengo la uhamasishaji na kuyaunganisha makundi ya vijana, Wanawake na watu wazima kushiriki katika shughuli za kiuchumi na Uzalishaji Mali, Uzalendo na Uwajibikaji ili kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla.
Amesema Jamii Mpya imeamua kufanya Uzinduzi huo kwa kuandaa bonanza la michezo ikiwa ni sehemu ya Shughuli zinazofanywa katika kila Uzinduzi ikiwa ni pamoja na kufanya usafi hata kuwatembelea wagonjwa katika hospitali mbalimbali hivyo Bonanza la michezo ni sehemu ya kuwakutanisha vijana wengi kama ilivyo lengo la kuanzishwa kwa Jamii Mpya.
Vijana ndiyo wasemaji wa kuu na ndiyo watendaji wakuu katika nchi hii tunaamini haya tuliyozungumza ambayo yanafanyika katika nchi yetu kupitia Uzinduzi huu vijana hawa watakua mabalozi wazuri wa kuweza kwenda kuyatangaza huko nje ambapo vijana hawa wanatokea. Amesema Bi.Somji
Amesema vijana walioshiriki bonanza hilo washindi watapatiwa zawadi baada ya bonanza hilo.
Post A Comment: