MBUNGE wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) James ole Millya amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Arusha.
Miongoni mwa waliojitokeza kuwania nafasi hizo ni Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki(EALA) James ole Millya na huku mfanyabiashara maarufu wa Jijini Arusha Hussein Gonga na wengine wanne ambao wamekwenda Ofisi ya CCM Mkoa kimya kimya kukabidhiwa fomu na sekretari wa chama ambaye hakupenda kutaja jina lake baada ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha,Mussa Matoroka kuwa kwenye ziara ya Utelelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoani.
Amesema yeye ni mbunge wa EALA lakini ameona ni vema agombee nafasi hiyo ili kuusaidia Mkoa wa Arusha ambao ni lazima uwe na timu imara kuhakikisha chaguzi zijazo chama kinashinda
Amesema yeye ni kijana aliyepikwa na chama amejitoa kuwania nafasi hiyo ili kusaidia chama kushinda kwani anajua vema siasa za nchi ya Tanzania
CCM imetangaza nafasi mbalimbali na mwisho wa kuchukua fomu ni Machi 25 mwaka huu ,awali nafasi hiyo ya ilifutwa na Katibu Mkuu wa CCM,Daniel Chongolo Novemba 21 mwaka jana baada ya kugubikwa na tuhuma za rushwa kwa Mkoa wa
Post A Comment: