MFANYABIASHARA maarufu mkoani Arusha anayejihusisha na biashara ya madini ikiwemo Tanzanite, Hussein Gonga ameamua kujitosa kuwania Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Mkoa wa Arusha kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Akithibitisha hilo yeye kwa njia ya simu skies nje ya Nchi,Gonga alisema amefanya uamuzi huo yeye mwenyewe kwa lengo la kukijenga chama ngazi ya Mkoa na sio vinginevyo.
Gonga ambaye amekuwa akikisaidia chama ngazi ya Wilaya na Mkoa pindi anapohitajika huenda kuingia ndani ya chama kukampa nafasi Nzuri ya kukijua Chama kwa undani zaidi tofauti na Awali akiwa nje ya chama.
Mwingine aliyejitosa kuwani nafasi hiyo ni pamoja na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM) ,Jemes Ole Millya na pia kwa Sasa ni Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Post A Comment: