Meneja wa uwanja wa CCM Mkwakwani Nassoro Makau 'Nassa' akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya fainali ya mchezo wa kombe Shirikisho la Azam utakaochezwa katika dimba hilo.
Na Denis Chambi, Tanga.
Mkoa
wa Tanga umepokea kwa furaha kubwa taarifa za kutangazwa kuwa mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho la Azam utachezwa katika dimba la CCM Mkwakwani kwa msimu huu wa 2022/2023.
Meneja
wa uwanja CCM Mkwakwani Nassoro Makau 'Nassa' alisema wamepokea kwa
bashasha taarifa hizo kuona kwamba uwanja wao unakidhi vigezo vya kuchezwa fainali
hizo huku akiahidi kwenda kuyafanyia marekebisho baadhi ya maeneo ambayo
bado hayajakaa sawa kulingana na hadhi ya mashindano hayo.
"Hii
ni fursa kubwa sana ambapo tunategemea kupata mashabiki wengi kutoka
wilaya za mkoa wetu na kutoka mikoa mingine tofauti tofauti kuja kuangalia fainali hii
katika mkoa wetu wa Tanga kwetu ni fursa kubwa , kuna viwanja vingi
sana lakini huu ndio umechaguliwa hatuwezi kukubali fursa hii itupite"
"
Toka kuanza kutangazwa kwa uwaja wa Mkwakwani kwetu huu ni mkakati namba moja kwa maana ya
kwamba zile sehemu zote ambazo ni korofi kwa upande wetu sisi tunapaswa
kuzishughulikia ipasavyo katika eneo la Pitch tutaendelea kuliboresha
na mengine kwa sababu fainali hii ni kubwa tutakaa kama kamati kuona
baadhi ya maeneo gani ambayo tuweza kuanza nayo lakini pia
kuyashughulikia ndani ya wakati" alisema Nassa.
Alisema
kuwa licha ya wapezi mashabiki na wadau wa soka kupokea taarifa hizo
kwa furaha itakuwa pia ni fursa ya kipekee siku hiyo itakayofungu
mlango kwa watu mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara kutokana na uwepo wa watu tofauti wa kutoka
nje na ndani ya mkoa huo.
"Licha
ya Mashabiki wengi kuja Mkwakwani kushuhudia fainali hizi lakini pia ni
fursa kwa watu wengine wakiwemo wafanyabiashara, watu wa usafiri,
wauzaji wa vyakula pamoja na wengineo wengi kila mwana Tanga kwa namna
yake ni fursa kwake. Alisema Nassa.
Hatua
ya robo fainali ambayo itaanza kuchezwa March 31 hadi april 2,2023 kwa timu ta Simba
SC kukutana na Ihefu , Azam FC wao watachuana na Mtibwa Sugar Singida
wakiminyana Mbeya City na mchezo wa mwisho utawakutanisha Yanga SC
dhidi ya Geita Gold kutafuta tiketi ya kutinga nusu fainali..
Post A Comment: