Mbunge wa Jimbo la Nachingwea DR Amandus Chinguile akifurahia jambo na mwananchi wa Jimbo hilo baada ya kusikia neema ya maji kuwa itawafikia

Na Fredy Mgunda, Nachingwea.


MBUNGE wa Jimbo la Nachingwea Dr Amandus Chinguile Mkoani Lindi amedhamilia kutatua changamoto za maji na afya kwa wananchi wa Jimbo hilo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kuwasikiliza wananchi,Dkt Chinguile alisema kuwa Wananchi wamekuwa wanatafuta maji mbali na maeneo wanayoishi


Dkt Chinguile alisema kuwa lengo ni kuhakikisha anawatua ndoo akina mama wa Jimbo la Nachingwea ili kuwawezesha kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo na sio kwenda kutafuta maji mbali au kutumia maji yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu

Alisema kuwa suala la maji limekuwa likimuumiza kichwa ndio maana akashirikiana na serikali kuhakikisha wanatafuta mradi mkubwa wa kutatua kero hiyo ya wananchi iliyodumu kwa miaka mingi.

Dkt Chinguile alisema mradi wa maji vijiji 21 utasiaidia kumaliza kabisa kero za wananchi kwenye vijiji hivyo ambavyo vimekuwa vinachangamoto toka kuumbwa kwa dunia.

Alisema kuwa mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 120 kwa vijiji vya Nachingwea na Ruangwa mkoani Lindi ambapo tayari mkandarasi ameshasaini mkataba ambao utatekelezwa kwa muda wa miezi 26.

Dkt Chinguile alimazia kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kimaendeleo anayowaletea wananchi wa Jimbo la Nachingwea na Tanzania kwa ujumla.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: