Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali juu ya umuhimu wa elimu ya kilimo kwa wananchi wote wa wilaya hiyo
Na Fredy Mgunda, Nachingwea.
MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amepiga marufuku maafisa Kilimo kukaimu nafasi za utendaji wa Kijiji na kata bali wanatakiwa kutoa elimu ya kilimo kwa wananchi wote.
Mkuu huyo wa wilaya ya Nachingwea alimuagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Injinia Chionda Kawawa kuacha mara moja tabia ya kuwapangia majukumu mengine maafisa Kilimo wa wilaya hiyo.
Moyo alisema kuwa Wananchi wa wilaya ya Nachingwea wanatakiwa kupata elimu ya kilimo ili kuondokana na njaa ya mara kwa mara ambayo wamekuwa wanakumbana nayo.
Alisema kuwa ardhi ya Nachingwea inakubali kila aina ya zao hivyo hakuna haja ya wananchi kulalamika wanajaa wakati ardhi na nguvu wanazo za kutosha kufanya shughuli za kilimo na kujikomboa kiuchumi.
Moyo amewataka maafisa Kilimo kuacha tabia ya kukaimu nafasi ya mtendaji wa kijiji na kata kwa kuwa wanatakiwa wakatimize majukumu ya kutoa elimu ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara katika wilaya hiyo.
Alisema kuwa Wananchi wa Nachingwea wanautajiri wa kutosha kutoka kwenye ardhi yao iliyobarikiwa kuwa na rutuba ambayo inakubali kilimo cha mazao yoyote yale.
Moyo alimazia kwa kuwataka maafisa Kilimo kuandaa ratiba maalumu ya kuwatembelea wakulima wa kila Kijiji kwa ajili ya kutoa elimu ya kilimo na ratiba hiyo apewe nakala ofisini kwake.
Post A Comment: