Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, akiwa amekalia kigoda wakati akihudhuria mkutano wa Shina namba 2 katika Kijiji cha Mntinko Wilaya ya Singida ikiwa ni muendelezo wa ziara yake mkoaniSingida ya kuangalia uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo ziara alyoifanya Machi 3,2023.
Na Dotto Mwaibale, Singida
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewataka Wazazi na Walezi nchini kusimamia na kuwaelekeza vijana wao kuzingatia suala la maadili hasa katika uvaaji wa mavazi yenye staha.
Chongolo ameitoa kauli hiyo Wilaya ya Singida katika Kijiji cha Mtinko, baada ya Mzee Emmanuel Mgoya kuelezea kukithiri kwa kumomonyoka kwa maadili kwa watoto wa kike na kiume katika kikao cha Shina namba 2 ambacho alikihudhuria.
"Katibu Mkuu wa CCM hivi sasa hali imekuwa mbaya Wanawake wanavaa nguo zisizo na staha hali hii inanikera sana nakuomba ukamwambie Rais Samia Suluhu Hassan kuwa uku kwetu wanawake hawavai mavazi yenye staha" alisema Mngoya.
Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo akizungumza baada ya kuelezwa jambo hilo alisema waasisi wa taifa letu waliijenga nchi kwa misingi ya maadili, ambapo Wazazi na Walezi walitakiwa kuhakikisha wanasimamia maadili ya watoto wao ili kuenenda vyema na utamaduni wa kitanzania.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter
Serukamba alisema tangu katibu mkuu huyo kuanza ziara
mkoani hapa baadhi ya maagizo aliyotoa yameanza
kutekelezwa ndani ya siku nne tangu ayatoe ambapo alitaka yatekelezwe
kabla hajamaliza ziara yake mkoani hapa.
Serukamba alitoa maelezo hayo katika mkutano wa Shina
namba mbili uliofanyika Kata ya Mntinko wilaya ya Singida ambapo Chongolo
alikuwa akisikiliza kero za wananchi.
Alisema Chongolo alitoa maagizo hayo
kwa nyakati tofauti wakati wa ziara hiyo ambapo akiwa wilayani Manyoni mmoja wa
wananchi alielezea kero ya barabara mbili za mitaa wilayani humo kutotengenezwa
kwa muda mrefu jambo lililokuwa likileta usumbusu kwa watumiaji..
"Katibu mkuu napenda kukueleza
kwamba maagizo yako yote uliyotuelekeza tumekwisha yafanya zile barabara mbili
za Manyoni tayari zimesembuliwa,saruji kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi imekwisha
nunuliwa na vituo vya kuchotea maji vikiwa vimefungwa na maji yameanza
kutoka" alisema Serukamba.
Jambo jlingine alilolitolea maagizo
ni ununuzi wa saruji kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa CCM wa wilaya hiyo ambapo
alitoa fedha kwa ajili ya kununua saruji mifuko 200 huku Mkuu wa Mkoa wa
Singida, Peter Serukamba na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemirembe Lwota wakitoa
ahadi ya kuchangia ujenzi huo mifuko 100.
Changamoto nyingine iliyotolewa ni kukosekana
kwa maji katika Kijiji cha Ulyampiti kilichopo Kata ya Unyahati ambacho pamoja
na maji kuchimbwa lakini yalishindwa kuwafikia wananchi kwa sababu ya
kutofungwa vituo vya kuchotea majiambavyo gharama yake ilikuwa ni Sh.milioni
1.2 fedha ambazo zilipatikana kwa yeye kutoa Sh.Milioni 1 na mkuu wa mkoa kutoa
Sh.200,000 ambapo aaliagiza kabla ya kumaliza ziara yake kazi hizo zimwe
zimekamilika.
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ramadhani Ighondo alitumia ziara hiyo kumuomba Chongolo asaidie ujenzi wa barabara ya lami ya kiwango cha lami ya kilometa 93 kutoka Singida mjini kupitia makao makuu ya wilaya hiyo Ilongero hadi Hydom mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akihutubia wakazi wa Kijiji cha Ngimu, Kata ya Ngimu, Wilaya ya Singida ikiwa sehemu ya ziara ya kuimarisha chama pamoja na kukagua, kuhimiza na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.
Post A Comment: