Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa,Daud Yassin amesema chama hicho kinathamini kazi ya bodaboda inayofanywa na vijana katika Mkoa huo.
Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Iringa ameyasema hayo wakati alipokutana na viongozi wa umoja wa waendesha bodaboda mjini Iringa.
Ndugu Yasin amesema kimsingi CCM inatambua uwepo wa bodaboda na kwamba ni kazi inayowaingizia kipato vijana Kama zilivyo kazi nyingine.
Amewaeleza viongozi hao kwamba, rai ya CCM kwa vijana wanaoendesha vyombo vya moto nii kufuata taratibu na sheria zote zilizopo katika utekelezaji wa majukumu yao.
"Sisi Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa! Tuko pamoja nanyi, lakini hakikisheni mnafuata taratibu zote na sheria Katika utekelezaji wa majukumu yenu," amesema na kuongeza;
"Waambieni vijana wenzenu kwamba ni muhimu kufuata taratibu na sheria zote zilizopo katika kuendesha vyombo vya moto, zikiwemo bodaboda. Endesheni kwa kufuata sheria, ili kulinda maisha yenu na maisha ya abiria mnaowapakia,"
Kwa upande wao viongozi wa umoja wa waendesha bodaboda mjini Iringa, wamemshukuru Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa kwa kuwaalika, na wametoa maoni na ushauri mbalimbali.
Kutokana na maoni na ushauri huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa ameahidi kufikisha ushauri wao kwa wahusika ili kuboresha shughuli hizo za vijana wa bodaboda.
Post A Comment: