Serikali imetenga shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji mkoani Arusha ambapo utekelezaji wa miradi hiyo umefikia asilimia 98.
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi ameyasema hayo wilayani Arumeru alipoambatana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye ziara ya kikazi.
Mahundi amesema Wizara ya Maji imetenga jumla ya shilingi milioni 650 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji wa USA River ambapo utakamilika mwaka wa fedha ujao.
Amempa wiki mbili Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Arusha kufanya marekebisho ili wananchi wapate maji safi na salama.
Aidha Mahundi amesema Wizara imeelekeza jumla ya shilingi bilioni 8 zitaondoa kabisa changamoto za Maji Arumeru.
Mahundi amemshukuru na amemhakikishia Rais Samia kuwa miradi yote itakamilika ili dhamira ya kumtua mama ndoo kichwani inakalika.
Post A Comment: