Na Denis Chambi, Tanga.
Milango
ya kibiashara na kiuchumi hapa nchini kupitia bandari ya Tanga inazidi
kufunguka hii ni mara baada ya Meli yenye ukubwa wa mita 189.9 kutia
nanga hivi karibuni ikitokea Marekani katika bandari ya Portlex ikiwa
imebeba shehena ya malighafi aina ya Petcoc tani 51 kwaajili ya
viwanda vya Sayona na Neelkanth vilivyopo jijini Tanga.
Kufwatia
maboresho yaliyofanywa na serikali yaliyoghalimu Jumla ya shilingi
bilioni 429.1 zilizotumika katika mradi wa maboresho ya gati mbili
zenye urefu wa mita 450 na kuongeza kina cha bahari kwa lengo la
kuiwezesha bandari hiyo kuhudumia meli kubwa ambazo awali hazikuweza
kushusha mizigo moja kwa moja bandarini hapo kutokana na kina kidogo.
Maboresho
hayo yaliyofanyika ambayo ni gati mbili zenye urefu wa mita 450
zilizojengwa miaka ya 1914 na 1958 pamoja na kuongeza kina cha bahari
kutoka mita 13 hadi13 ambazo sasa zinawezesha meli kubwa mbili na
kuhudumiwa kwa wakati mmoja.
Akizungumza
mara baada ya kuipokea Meli hiyo mkuu wa kitengo cha masoko katika
bandari ya Tanga Rose Tandiko amesema kuwa Meli hiyo ya MV Motsovo ya
mizigo ni kubwa zaidi ya zile ambazo zilishawahi kupokelewa bandarini
hapo na bado wanaendelea kupokea nyingine akitumia nafasi hiyo
kuwakaribisha wadau na wafanyabiashara wa ndani na nje ya Tanzania
kuendelea kuitumia bandari hiyo
"Leo
tumepokea meli kubwa kuwahi kuhudumiwa katika bandari yetu ya Tanga
ambayo imekuja kutokea nchini Marekeani ikiwa na mzigo wa Petcoc tani
elfu 51 kwaajili ya viwanda vya Neelkanth na Sayona limited, huu n
mwanzo tu wa huduma zilizotukuka katika bandari ya Tanga bado
tutaendelea kuhudumia meli nyingine mbili kubwa gatini kwa wakati mmmoja
kama matakwa ya ujenzi wa gati letu"
"Tuwahamasishe
wadau wa bandari ya Tanga, wadau wa bandari zote hapa nchini na
kweingineko kwamba endeleeni kutumia bandari yetu bandari ya Tanga kwa
sasa tunaweza kusema imenoga huduma zimetukuka na utendeaji kazi ni
mzuri hivyo tunawakaribisha sana kutumia bandari yetu ya Tanga" alisema
Tandiko.
Meli hiyo
iliyopokelewa bandarini Tanga march 18 ilitokea katika bandari ya
Portlex nchini malekani february 3, 2023 kwaajili ya kuleta shehena hiyo
ya Petcoc inatoyumika kwenye viwanda vya Sayona na Neelkanth kama
chanzo cha moto wa viwandani
Meneja
usafirishaji kutoka kampuni ya Seif Issa MR & SONS ambao ni
miongoni mwa wadau wa bandari ya Tanga ameipongeza serikali kwa
uwekezaji mkubwa uliofanyika katika kuboresha na kuweka mazingira kwa
rafiki kwa wafanyabiashara wanaotumia bandari hiyo wa kutoka nje na
ndani ya nchi ambapo itawasaidia kwa kiasi kikubwa tofauti na hapo
awali.
"Tunataraji
utendaji kazi mzuri kwa sababu kila idara imejipanga kuanzia wafanya
kazi na vitendea kazi kwahiyo tunategea tufanye kazi kwa siku ambazo
tumepangiwa , wafanyabiashara wasihofie wala kuogopa tunaamini bandari
iko salama kabisa kila kitu wamekiweka katika mpangilio mzuri kwahiyo
wadau wengine tunaomba waitumie bandari ya Tanga" alisema Issa.
Tangu
kufanyika kwa maboresho ya ukarabati wa gati mbili na upanuaji wa kina
cha bahari bandari hiyo imeendelea kuvunja rekodi za kupokea meli kubwa
za mizigo kutoka nje ya nchi ambapo kabla ya Mv Metsovo zilitia nanga
meli zenye urefu Mita 150, na 179 kwa nyakati tofauti tofauti hii
ikiendana na kauli ya Tanga lango kuu la uchumi Afrika mashariki.
Post A Comment: