Halmashauri 14 nchini zimepata hati zenye mashaka baada ya ukaguzi uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, huku Ushetu ikipata hati chafu.


Hayo yamebainika wakati uwasilishaji wa ripoti ya mkaguzi huyo na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali uliofanyika jana Machi 29, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mbali na Halmashauri vipo vyama vya siasa ikiwemo Sau na Demokrasia makini, mashirika ya umma.


Akitaja halmashauri zilizopata hati zenye mashaka ni Arusha DC, Babati DC, Bahi DC, Geuta DC, Geita DC, Geita TC, Kilindi DC, Mbinga TC, Musoma DC, Nkasi DC, Nyasa DC, Simanjiro DC, Songwe Dc, Sumbawanga Mc na Ushetu iliyopata hati mbaya.

Katika vyama vya siasa, Chama cha Sau kilipata hati chafu, Demokrasia Makini, UDP, Chama cha wakulima zote zilipata hati zisizoridhisha.

Katika mashirika ya umma ni Magazeti ya Serikali, Kampuni ya mbolea, mamlaka ya maji safi   na usafi wa mazingira Nzega, Korogwe na Kyela-Kasumuru, Taasisi ya Mifupa Muhimbili, Shirika la Masoko ya Kariakoo.

"Hizi mbili kwa maana ya Kasumuru na Shirika la Masoko Kariakoo nilishindwa kutoa maoni," amesema Kichere.

Kwa upande wa Serikali Kuu, wakala wa ufundi na umeme walipata hati mbaya, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tarime daraja C ilipata hati yenye mashaka, Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wote walipata hati zenye mashaka.

Katika vyama vya siasa, Chama cha SAU kilipata hati mbaya, Demokrasia Makini, UMD, UDP vilipata hati zenye mashaka huku Chama cha Wakulima (AFP) alishindwa kutia maoni.

Hati hizo ni kati ya 1,045 zimetolewa ambapo 218 ni za tawala za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, 203 mashirika ya umma, 315 ni serikali kuu, 19 vyama vya siasa na 290 ni za miradi ya maendeleo.


Kati ya hati hizo asilimia 90 hati zinazoridhisha ni 1,010, 29 zinashaka, hati mbaya tatu na 3 za kushindwa kutoa maoni.

Share To:

Post A Comment: