Na Fredy Mgunda,Iringa.
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Iringa inashirikiana na chuo cha Iringa kupitia kitivo cha utalii na anthropolojia katika kuvitangaza vivutio vya utalii pamoja na kuhamasisha wananchi kupenda kutembelea vivutio vya ndani.
Akizungumza na waandishi wa habari,afisa kutoka ofisi ya utalii Kanda ya Iringa Hoza Mbura alisema kuwa zaidi ya wanafunzi 50 wa chuo kikuu cha Iringa kitivo cha utalii na anthropolojia wamefanikiwa kutembelea vivutio vya utalii wa ndani vya nyanda za juu kusini mwa Tanzania ambavyo vitawasaidia katika masomo yao.
Mbura alisema kuwa wamefanya kampeni ya kuhamasisha wanafunzi kutembelea vivutio vya utalii vya ndani ili kuongeza idadi ya wananchi ambao hawajui umuhimu wa utalii.
Alisema kuwa wamefanikiwa kutembelea vivutio vya mkoa wa Njombe na Mbeya ambavyo ni vivutio vya utalii vya Mpanga kipengere,Ziwa Ngosi,Fukwe za Matema pamoja na daraja la Mungu ambavyo vinavutia wananchi wote wa ndani na nje ya nchi.
"Faida kubwa waliopata wanafunzi kwanza ni kujifunza juu ya vivutio vinavyopatikana kusini mwatanzania,Pia wameondoka na experience isiyosahaulika kwani wengi ndio mara ya kwanza kufika katika vivutio hivyo"alisema Mbura
Mbura alisema kuwa faida waliyoipata kujifunza kwa vitendo juu ya vivutio vya utalii vya ndani na kulinganisha na kile wanachofundishwa darasani na uhalisia wake katika mazingira husika ambayo itawasaidia katika masomo yao.
"Lengo nikuhamasisha utalii wa ndani kupitia kampeni maalumu ya shule za msingi sekondari na vyuo vya elimu"
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imehitimisha kampeni ya kutangaza,na kuhamasisha utalii wa ndani kupitia vivutio vya utalii vilivyopo Njombe na Mbeya ambapo zaidi ya wanafunzi 50 wa chuo kikuu cha Iringa kitivo cha utalii na anthropolojia walihamasika kutembelea vivutio hivyo wakiwa sambamba na maafisa wa ttb kanda ya iringa.
Wametembelea vivutio vya daraja la mungu God's Bridge,daraja kubwa la asili lililounganishwa na kingo mbili za mto kiwira wilaya ya Rungwe takribani kilometa 10 upande wa magaharibi mwa tukuyu,
Post A Comment: