Na;Elizabeth Paulo ,Dodoma
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeendelea kuandaa na kuratibu mafunzo kwa viongozi, Wadhahiri na maofisa wa vyuo vikuu vya umma na binafsi nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo katika usimamizi na uendeshaji wa taasisi zao.
TCU imeendelea kuwajengea uwezo Wadhahiri na viongozi wa vyuo vikuu kuhusiana na utolewaji wa elimu ya chuo kikuu ikiwa ni moja ya majukumu yake kama ilivyoainishwa katika Sheria ya vyuo vikuu sura ya 346 ya sheria ya Tanzania ambapo katika kipindi cha julai-Desemba,2022 jumla ya viongozi na wanataaluma 575 wamenufaika na
mafunzo hayo yaliyolipiwa na serikali kwa asilimia 100.
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles D. Kihampa alipokua akielezea utekelezaji wa majukumu ya Tume kwa miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya awamu ya Sita mbele ya waandishi wa habari.
“Kuanzia mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 6.4 kupitia mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi kwaajili ya kuimarisha uthibi ubora na uhuishaji wa mitaala ya vyuo vikuu ambapo zaidi ya mitaala 300 ya vyuo vikuu iko katika hatua mbalimbali za kufanyiwa mapitio ili kuhuishwa kwa kuzingatia maoni ya wadau mbalimbali ili kukidhi matarajio Yao na mahitaji ya solo.”Alisema Prof.Kihampa
Prof. Kihampa amesema Serikali imeendelea kutekeleza kwa vitendo azma ya kuongeza wigo wa fursa za masomo ya elimu ya juu kwa watanzania ambapo katika kipindi cha miaka miwili fursa mbalimbali za masomo zimeongezeka.
Akizungumzia suala la udahili wa wanafunzi , katika shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2022/23 ni 113.383 ukilinganisha na mwaka 2020/21 ambapo ulikuwa ni 87,934 ambapo ongzeko hilo ni sawa na asilimia 28.9 ,ongeko hilo likichagizwa na kuongezeka kwa fursa za masomo ya elimu ya juu na idadi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu nchini.
Katibu Mtendaji huyo amesema kuwa kutokana na kuimarishwa kwa programu za elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Elimu ya Chuo Kikuu, imesaidia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu majukumu ya TCU na taratibu za uendeshaji wa elimu ya chuo kikuu na kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto wanazokutana nazo wanafunzi na wadau wengine wa elimu ya juu katika kipindi cha hivi karibuni ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita.
Katika kipindi cha Mwaka 2022/2023 TCU imepokea barua 5 za maombi kujengwa vyuo vikuu baada ya serikali kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji Kadhalika Serikali inatarajia kujenga vyuo vikuu 14 sambamba na elimu bila malipo.
Amesema kuwa TCU imeweka utaratibu wa kuanzishwa na kuimarishwa mifumo ya uthibiti ubora ndani ya vyuo vikuu ambapo vyuo vyenyewe vimekuwa na utaratibu wa kujikagua,kujitathmini na kufanya marekebisho mbalimbali kwa kuzingatia miongozo ya uendeshaji wa vyuo vikuu.
"kwa mfano, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari ,2023 vyuo vikuu vyote 47 vilivyopo vimekaguliwa na kupewa ushauri wa maeneo yanayohitaji kuboreshwa, na zoezi hili la ukaguzi wa vyuo ni endelevu kila mwaka"amesema Prof.Kihampa
Kwa upande wake Msemaji mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa amesema Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya kiuchumi ni kati ya miradi mikubwa iliyopatika ndani ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita ambapo jumla ya trilioni moja iliyopatikana kwa mkopo wa benki ya Dunia zitakwenda kutumika kuboresha elimu ya juu ikiwemo TCU kupata bilioni 6.4.
Msigwa amesema Mradi huo unatarajiwa kufikia mikoa 14 kwa kujenga matawi ya vyuo vya elimu ya juu ili kuwasaidia watanzania walioko kila mkoa wasilazimike kwenda mbali kutafuta elimu ya juu na kupata elimu ndani ya mkoa husika katika tawi la Chuo kikuu .
“Leo kuna watanzania wengi vijijini wangetamani kupata elimu ya juu lakini vyuo viko mbali akijumlisha garama za kuishi, usafiri, unaweza ukaziona kama ni ndogo lakini ni mambo ambayo yanawakatisha tamaa na yanapelekea wengi kukosa haki yao ya Elimu ya juu kwasababu sasa Serikali imeweka utaratibu wa kila mtanzania akifikia elimu ya juu anauhakika wa kupata mkopo.”Alisema Msigwa Na Kuongeza
“Na mimi kila siku nasema Tanzania sasa usipokua na Degree umetaka tu Mwenyewe kwasababu unasoma shule ya msingi bila malipo,Secondary bila malipo na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Ameongezea kidato cha Tano na Sita bila malipo ukienda chuo kikuu kuna mikopo kwaajili yako sasa wewe mwenyewe utake kutokupata Degree lakini Degree zinapatikana.
Post A Comment: