Na John Walter-Manyara
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema chini ya mipango iliyopo katika awamu ya sita watahakikisha jengo la ofisi ya makao makuu ya polisi mkoa wa Manyara linakamilika.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa jeshi la Polisi, Magereza pamoja uhamiaji mkoa wa Manyara alipofanya ziara ya kikazi na kukagua mradi wa jengo la ofisi ya uhamiaji na Polisi yanayojengwa katika mji wa Babati.
Amesema atafanya mchakato deni la shilingi Milioni 62.8 linalodaiwa na mkandarasi lilipwe ili ujenzi huo uliosimama kwa muda mrefu uendelee.
Jengo hilo ambalo limenza kujengwa tangu mwaka 2010 kwa muundo wa orofa, halijaendelezwa na badala yake limeishia katika hatua ya msingi kwa zaidi ya miaka 12.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara George Katabazi amemweleza Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni kwamba ujenzi wa mradi wa jengo la ofisi ya Polisi mkoa wa Manyara ulianza mwaka 2010 chini ya mkandarasi Stance Technic And Civil Engineering.
Amesema Mkataba wa Ujenzi ulisainiwa kati ya Wizara ya mambo ya ndani na Stance Technic And Civil Engineering ambapo ulikuwa na thamani ya shilingi Milioni 581.3.
Ameeleza kuwa Mkandarasi anaidai jeshi la polisi shilingi milioni 62.8 kwa ajili ya kuvunja mkataba ili jengo liendelee kujengwa kwa mfumo wa Force Account.
Mbunge wa jimbo la Babati Mjini ambaye pia ni Naibu waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Paulina Gekul amemshukuru Waziri kwa kufika kukagua ujenzi wa jengo hilo akisema inaleta matumaini kwa jeshi la polisi ambao wana kazi kubwa ya kulinda raia na mali zake.
Mbunge wa jimbo la Babati Mjini ambaye pia ni Naibu waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Paulina Gekul amemshukuru Waziri kwa kufika kukagua ujenzi wa jengo hilo akisema inaleta matumaini kwa jeshi la polisi ambao wana kazi kubwa ya kulinda raia na mali zake.
Post A Comment: