Na John Walter-Manyara
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua kali dhidi ya Mkandarasi ambaye anatelekeza ujenzi wa mradi wa ofisi ya Uhamiaji mkoa wa Manyara kwa kushindwa kukamilisha ujenzi kwa muda.
Waziri Masauni ametoa agizo hilo leo Februari 4, 2023 wakati akikagua mradi wa ujenzi wa ofisi ya jengo la uhamiaji mkoa wa Manyara ambapo amesema Serikali inalipa fedha nyingi kwa ajili ya wananchi kupata huduma.
Ujenzi wa jengo hilo la uhamiaji hadi kukamilika kwake inatajwa kutumia shilingi Bilioni 1.8.
Aidha amemuomba radhi Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutokamilika kwa wakati mradi huo kama alivyomuahidi mbele ya wananchi uwanja wa Kwaraa alipokuwa akizungumza na wakazi wa mjini Babati.
Post A Comment: