Na Imma Msumba ; Monduli
Ripoti ya usawa katika fursa ya kupata maji safi ya kunywa na masuala ya usafi na kujisafi inaonyesha kwamba zaidi ya nusu ya watu wote duniani hawana fursa ya kupata huduma salama za usafi.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa mwaka juzi kwa ushirikiano wa shirika la afya duniani WHO , na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, mabilioni ya watu duniani wanaendelea kutaabika kutokana na kukosa huduma bora za maji na masuala ya usafi.
Takribani watu bilioni 2.2 kote duniani, ripoti inasema hawana huduma ya maji salama ya kunywa, bilioni 4.2 wengine hawana huduma salama za usafi na wwatu bilioni 3 wanakosa huduma za msingi za shemu za kunawa mikoni.
Nchini Tanzania katika Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha matumizi ya maji ya Bwawa huenda yasifikie kikomo kwa matumizi ya Binadamu kutokana na jiographia ya Wilaya hiyo kuwa na Changamoto kubwa ya upatikaji wa Maji safi na Salama.
Wananchi na wakazi wa kata ya Naalarami ambapo wakina Mama ndio Waathirika zaidi ya changamoto hiyo kutokana na kutembea umbali mrefu kufata Maji ya matumizi ya nyumbani ambapo Maji hayo ni ya mabwawa yanayotumiwa na mifugo na binadamu.
Mary Mollel ni Mkazi wa kata ya Naalarami anaeleza kuwa ukosefu wa maji safi na salama ni changamoto kubwa kwao hali inayopelekea kuwa na matumizi makubwa ya maji ya mabwawa
"Ukweli usiopingika ni kwamba kata yetu ya Naalarami tuna shida sana ya maji safi na salama hali ambayo inapelekea tuwe na matumizi makubwa ya maji ya mabwawa , lakini Cha ajabu mabwawa yenyewe hatuna yaliyopo ni machache na yako mbali , unamkuta mama anaamka alfajiri ya saa kumi unaenda kufuata maji ambayo si salama wala safi kwa matumizi ya binadaamu na tushazoea hatuumwi, na ukirudi ndama wanangojea maji na pengine watoto wamekosa hata chai na shuleni hawajaenda ". Amesema Mary Mollel
Lemi Laizer ni Diwani wa kata ya Naalarami Wilayani Monduli, nae alithibitisha kuwa ni kweli kuna ukosefu wa maji safi na salama, na kwambi ni changamoto kubwa katika kata yake. Hali inayowaathiri zaidi Wamama kutokana na kutembea umbali mrefu kufuata maji bwawani na pengine Maji hayo ya bwawa yasipatikane kwa wakati kutokana na kuwepo kwa uchache wa mvua hususani kipindi hiki cha mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Monduli Selemani Yusuph Mwenda amesema Wilaya ya Monduli ina changamoto ya Upatikaji wa maji safi na salama kwa ujumla wake na hata Mabwawa yanayotegemewa yanakauka kutokana na uchache wa mvua.
Je chanzo cha ukosefu wa maji ni nini?
Pamoja na changamoto hizo, je nini kifanyike? Mary Mollel ni Mkazi wa kata ya Naalarami anasema;
"Niiombe Serikali yangu sikivu ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuangalia namna ya kuyachuja maji haya kwa ajili ya matumizi ya binadamu na pamoja na kuwaongezea wananchi hawa mabwawa ya kutosha na kama itawezekana kuwepo na mabwawa kwa ajili ya kunyweshea mifugo maji na mengine kwa ajili ya Matumizi ya Binadaamu tu watakuwa wameisaidia sana jamii ya kifugaji" .
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Selemani Yusuph Mwenda alieza mikakati ya serikali ni kusimamia miradi yote ya maji inayoendelea katika Wilaya hiyo kwa lengo la huduma hiyo kuwafikia Wananchi wote.
Post A Comment: