Na; Elizabeth Paulo, Dodoma
Serikali kupitia mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) imetenga kiasi Cha shilingi bilioni 199 kwaajili ya ujenzi wa minara ya Mawasiliano nchini ikiwemo maeneo ya Vijijini.
Mtendaji Mkuu wa mfuko wa Mawasiliano kwa wote Justina Mashiba ametasema hayo leo jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mfuko huo mbele ya waandishi wa habari huku akisema UCSAF imeingia mikataba kufikisha huduma katika kata 1,242 zenye vijiji 3,654, wakazi 15,130,250 ambapo minara 1,087 yenye vijiji 3,378 na wakazi 13,320,750.
Mashiba amesema utekelezaji unaendelea katika minara 155 yenye vijiji 276 na wakazi1,809,500 ikiwemo Mradi wa kimkakati Zanzibar, Minara 42 shehia 38 ruzuku TZS bilioni 6.9.
Akizungumzia hali ya Mawasiliano nchini Mashiba amesema kuwa Mwaka 2009 Population Coverage ya Huduma za Simu ilikuwa asilimia 45 (45%) wakati kwa sasa imeongezeka hadi kufikia asilimia 96 (96%),Teknolojia ya 2G coverage yake ni 96%,3G ni 72%,4G ni 55% na Geographical Coverage ya 2G ni 69%; 3G ni 55% na 4G ni 36%.
Aidha Mashiba ameeleza kuwa kwa kuhakikisha mfuko huo unafanikisha Mawasiliano mfuko huo unafikisha Mawasiliano kwa Watanzania waishio Vijijini na mara baada ya kukamilika kwa minara hiyo Watanzania takribani millioni 15 watafikiwa na Mawasiliano na kupata huduma za internet kwa Uhakika.
Katika hatua nyingine Mashiba amesema kuwa mfuko huo unatarajia kutumia shilingi 575,000,000 ,kwa ajili ya Mradi wa Kupeleka Vifaa Maalum vya TEHAMA vya Kujifunzia kwa Shule 16 Zenye watoto wenye mahitaji maalum hapa nchini.
Ambapo vifaa vitakavyopelekwa katika shule hizo ni pamoja na na TV, Braille Machine (Nukta Nundu) Orbit reader (Machine za Kisasa), Laptops, Embosser (Printa ya nukta nundu).
"Shule hizi 16 zitanufaika na naamini vifaa hivi vitakapowafikia hawa watoto wenye mahitaji maalum vitawasaidia katika kujifunza na kufikia malengo na nia ya mfuko wa UCSAF ni kuhakikisha nchi nzima inaunganishwa na mawasiliano,"amesema Mashiba
Mtendaji huyo ameongeza kuwa Jumla ya shule 811 zimefikishiwa Vifaa vya TEHAMA ambapo kwa wastani kila shule imepewa Kompyuta 5, Printa 1 na Projekta 1.
Kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, Shule 150 zitafikishiwa vifaa vya TEHAMA,Bajeti yake ikiwa ni TZS 1,950,000,000/- na vifaa hivyo vitasaidia wanafunzi kusoma katika shule hizo 811,"amesema MashibaAkizungumzia utoaji wa elimu kwa walimu juu ya uboreshaji wa matumizi ya TEHAMA ambapo mwaka 2016 mafunzo yalianza ambapo walimu 3,465 wamepatiwa mafunzo na walimu wapatao 3,139 wanatoka Tanzania bara na walimu 326 wanatoka Tanzania Zanzibar.
Hata hivyo UCSAF imeeleza kuwa katika mkakati wa kuhakikisha kila mtanzania anatumia huduma ya tehama wameanzisha mpanga wa kufunga mitandao ya wife katika sehemu za wazi kama vile vyuo vikuu,mahosipitali pamoja na kwenye masoko ili kila mmtanzania aweze kutumia mtandao nakupata huduma kwa wepesi.
Post A Comment: