Na;Elizabeth Paulo,Dodoma

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania(TEMESA) unaishukuru Serikali ya awamu ya 6 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi chini ya Waziri Prof.Makame Mbarawa na Katibu Mkuu Balozi Mha.Aisha S. Amour kwa kufanikisha Upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa miradi,Muongozo wa kisera,Usimamizi na Maelekezo ya mara kwa mara yanayowezesha wakala kutekeleza majukumu yake kwa mafanikio.


Katika mwaka wa fedha 2022/2023 serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi iliidhinisha bajeti yenye jumla ya shilingi bilioni 21.277 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) .

Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu (TEMESA) Lazaro Kilahala alipokutana na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akielezea Utekelezaji wa Majukumu ya Wakala katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita.

“Miradi hii inajunuisha Ujenzi wa Vivuko vipya serikali ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 4.5, Ukarabati wa wa Vivuko vinavyoendelea kutoa huduma shilingi 5.8, Ujenzi wa miundombinu ya Vivuko shilingi bilioni 3.3, Ujenzi wa karakana mpya shilingi bilioni 2.5, Ukarabati wa karakana shilingi bilioni 1, Ununuzi wa Vipuri na vitendea kazi shilingi bilioni 1.5 Ununuzi wa mifumo ya TEHAMA shilingi bilioni 2, Usimamizi wa Miradi na Mafunzo shilingi bilioni 435”.Alitolea ufafanuzi Kilahala


Wakala umesaini mikataba mitano (5) ya ujenzi wa vivuko vipya vya Kisorya-Rugezi, Ijinga-Kahangala, Bwiro-Bukondo,Nyakarilo-Komwe na Mafia -Nyamisati yenye thamani ya shilingi bilioni 33.2 ambapo Hadi kufikia mwezi January 2023 jumla ya shilingi billion 10.3 zimekwisha lipwa kama malipo ya awali na ujenzi wa Vivuko hivyo unaendelea, Aidha wakala unakamilisha taratibu za Ununuzi wa kivuko cha Buyagu -Mbarika na (Sea Tax) mbili.

Kilahala amesema Hadi kufikia mwezi January 2023 Wakala umesaini mikataba ya utekelezaji wa miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 71.96 ambapo jumla ya shilingi bilioni 23.65 zimekwishalipwa kati ya fedha hizo jumla ya shilingi bilioni 15.625 zimetolewa ndani ya serikali katika mwaka huu wa fedha kiasi kilichobako kitaendelea kulipwa kadiri utekelezaji unavyofanyika na hati za madai kuwasilishwa.


“Wakala katika mwaka wa fedha2022/23 ulijipanga kuzalisha jumla ya shilingi 90,435,876,240 kama mapato ghafi kupitia Shughuli zake za matengenezo na ufundi, Usimamizi wa Vivuko,Ukodishaji wa Mitambo na huduma za ushauri”.Alisema

Aidha amesema mpaka sasa nchini kuna jumla ya vivuko 32 ambapo kila baada ya muda lazima vitembelewe kufanyiwa ukarabati ili kuhakikisha vinakua na ubora wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi na wakala umesaini mikataba 16 ya Ukarabati wa Vivuko yenye thamani ya shilingi billioni 23.3 kati ya hizo mwezi January 2023 Serikali imekwishalipa 7.96 na Ukarabati wa Vivuko 6 umekamilika ambavyo ni MV. KAZI, MV.MUSOMA,MV.KILAMBO,MV.SABASABA,MV.TEMESA na MV.TANGA.

Kadhalika Kilahala amesema changamoto kubwa inayoikabili (TEMESA) ni nauli za vivuko ambazo ni nauli za miaka 10 iliyopita na haziendani na bei ya soko wala garama halisi za uendeshaji wa Vivuko.

Katika hatua nyingine amesema mahitaji ya Mafuta ya Dizeli kwaajili ya kuendesha vivuko vyote ni lita 210,000 kila mwezi ambapo kutokana na ongezeko la bei za mafuta imepelekea ongezeko la garama za uendeshaji takribani milioni150.

“Garama za uendeshaji wa hivi vitu come ongezeko, Mwaka uliopita wastani wa lita moja ya Dizeli peke yake iliongezeka kama shilingi Mia saba nakitu ndani ya mwaka mmoja, Licha ya serikali kufanya jitihada kubwa kuweka ruzuku kwenye Mafuta , Ruzuku ipo ipo lakini bado kuna ongezeko la shilingi takribani mia 700 kwa lita ”.Alisema na Kuongeza



“Ongezeko hilo pia linakuja kwenye Vipuli ambapo tulisherekea mwaka jana ongezeko la mishahara ya watumishi jambo jema lakini kwetu sisi kwasababu zaidi ya asilimia 80 ya watumishi wa Vivuko kutokana na makusanyo ya Vivuko hii pia ikawa ni changamoto kwahiyo tunaendelea na mazungumzo na Wizara lakini kusudio letu ni kwamba hizi nauli sasa ziangaliwe upya.”


Kutokana na malalamiko ya baadhi ya wateja wa (TEMESA ) kulalamikia garama kubwa ya utengenezaji wa magari Kilahala amesema Wakala katika kutekeleza jukumu la utengenezaji wa magari wananunua bidhaa(Spare part) kwa watu wa kati na wakala utaanza kununua Viwandani moja kwa moja hivyo wapo katika mchakato wa kuanza kuagiza katika viwanda vya nje ya nchi ili kuondoa kero hiyo kwa wateja wao.


TEMESA ilianzishwa chini ya sheria namba 30 ya mwaka 1997 chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kufanya matengenezo ya magari, Usimamizi wa mafundi umeme,Kukodisha mitambo TEMESA nchi nzima na kuisaidia serikali katika maeneo hayo.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: