Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Kilewela akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Uhamasishaji kwa Wauzaji wa chakula kwenye Mikusanyiko, Wasafirishaji wa chakula na wasagaji wadogo wa nafaka katika Mkoa wa Dar es Salaam ambayo yamefanyika leo Februari 2,2023.

***************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SAlAAM
Idadi ya watoa huduma ya Chakula katika mikusanyiko ambao wamekaguliwa maeneo yao na kupata vibali na Shirika la Viwango (TBS) si ya kuridhisha ikilinganishwa na idadi ya watoa huduma katika Jiji la Dar es Salaam.
Ameyasema hayo leo Februari 2,2023 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Kilewela wakati akifungua Mafunzo ya Uhamasishaji kwa Wauzaji wa chakula kwenye Mikusanyiko, Wasafirishaji wa chakula na wasagaji wadogo wa nafaka katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Amewataka wadau hao kuhakikisha wanasajili maeneo yao kwa mujibu wa sheria na pia kuwa mabalozi wema kwa wenzao wanaofanya shughuli hiyo kwenye maeneo mbalimbali.
Aidha Dkt.Kilewela amesema mafunzo hayo yamelenga kuwahamasisha wadau wao kwa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu kanuni, sheria na miongozo ya shirika katika kuhakikisha jamii inapata chakula bora na salama.
Post A Comment: