Na Denis Chambi, Tanga.
Uongozi wa Seneti ya vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Tanga umemshukuru na kumpongeza Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa hatua aliyoichukuwa ya kuongeza kiwango cha fedha za kujikimu (Boom) kwa wanafunzi wa elimu ya juu waliopo katika vyuo nchini mbalimbali hapa nchini kutoka kiasi cha shilingi elfu nane mia tano (8500 ) hadi elfu kumi (10, 000) kwa siku jambo ambalo limewapa faraja na ari katika masomo yao.
Pongezi hizo zinakuja kufwatia mkutano uliofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kukitana pamoja na viongozi wa shirikisho la vyuo vya elimu ya juu Tanzania bara 'TAHLISO' pamoja na wale wanaowakilisha visiwani Zanzibar 'ZAHLIFE' ambapo rais alitangaza neema hiyo iliyopokelewa kwa furaha na wanafunzi hao.
Akizungumza mwenyekiti wa Seneti mkoa wa Tanga Hamilton Ezekiel alimpongeza na kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa hatua hiyo sambamba na kuwapatia ofisi ya samani kwaajili ya kuendesha shughuli mbalimbali za umoja huo.
"Kwa heshima na taadhima nachukuwa fursa hii kumshukuru sana Rais wetu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake wa dhati kwa kukubali kuzungumza na sisi vijana wa vyyo na vyuo vikuu, shabaha ya Rais imeonekana kwetu, kwa niaba ya vijana wa Seneti mkoa wa Tanga ninabeba ajenda kwa kuyasema mazuri yanayofanywa na serikali ya Rais na nitaendelea kuwa mkarimani wa vijana wenzangu kwa yale yote yatakayofanywa na yaliyofanywa na serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hasaan, hakika ilikuwa ni siku ya kipekee na ni ya historia kubwa kwetu tuna deni kubwa kwake " alisema Ezekiel.
"Kwa niaba ya vijana wa Seneti mkoa wa Tanga tunakushukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kupandisha kiwango cha fedha ya kujikimu (Boom) kutoka shilingi elfu nane na mia tano hadi elfu kumi kwa siku asante sana Rais wetu, sisi kama vijana tuna deni kubwa sana la kwenda kuyasema mema yote na kazi kubwa unayoifanya katika nchi yetu ya Tanzania"
Pamoja na pongezi mwenyekiti huyo ameiomba serikali kwa kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 kungalia namna ya kuwasaidia fedha za kujikimu wanafunzi waliopo vyuooni katika ngazi ya cheti na astashahada ombi ambalo pia lilipokelewa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Post A Comment: