Na Mwandishi Wetu, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter
Serukamba amewaagiza waratibu wa UKIMWI nchini
kuzungumza na jamii kwa uwazi kuhusu mabadiliko ya tabia katika
kujikinga na maambukizi ya VVU ifikapo 2030 kuwe na Tanzania isiyokuwa na
UKIMWI.
Akizungumza leo Februari 20,2023 wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa
taarifa ya mapitio ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na sekta binafsi ya
mwaka 2022 iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana aalisema iwapo jamii itaelewa
vizuri na ikakubali kubadili tabia Tanzania itafikia malengo ya Dunia ya 2030
ya kumaliza UKIMWI.
Serukamba alisema kuwa Serikali imekua ikipambana kudhibiti maambukizi ya
VVU pamoja na madhara yake kwa zaidi ya miaka thelathini, ambapo kwa kiasi
kikubwa mapambano haya yanategemea fedha kwa ajili ya utekelezaji wa afua za
UKIMWi,ambapo amefafanua kuwa kwa mahitaji kwa mwaka ni takribani Sh. Trilini
1.3.
Aidha, aliongeza kuwa utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI umekua ukipata
fedha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali hivyo ni muhimu kufanya mapitio ya fedha
zinazotumika kwenye afua hizo ili kubaini mchango wa taasisi za sekta ya umma
na mchango wa taasisi za sekta binafsi ikiwa ni pamoja na kutambua Maeneo
ambayo mchango huo unapelekwa kulingana na afua za VVU na UKIMWI lakini muhimu
zaidi kutambua upungufu uliopo wa fedha katika kutekeleza afua za VVU na UKIMWI
hapa ili Kuhakikisha utekelezaji wenye tija kwa Taifa, Jamii na mtu mmoja
mmoja.
Akifafanua umuhimu wa kufanyika kwa zoezi la Mapitio ya Fedha za UKIMWI
kwenye Sekta ya Umma na Binafsi (Public and Private Expenditure Review) ni kuwa
zinaisaidia serikali kufahamu kiwango cha matumizi ya fedha za UKIMWI
kinachopangwa na Sekta ya Umma na Binafsi.
Pia kufahamu maeneo ambayo fedha hizo zinaelekezwa, kujua kiwango cha
utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI ili kubaini mchango wa sekta ya umma na
binafsi katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI. Aidha, mapitio ya fedha za
UKIMWI husaidia kubaini changamoto katika utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI
nchini na kuweka mikakati ya kuzitatua.
Serukamba ameyataja mafanikio ya mafanikio yaliyotakana na zoezi hilo kuwa
ni pamoja na kuboresha ugawaji wa rasilimali fedha za UKIMWI kulingana na afua
zinazotekelezwa hapa nchini, kuimarisha mikakati ya kuhamasisha sekta binafsi
na sekta za umma kupanga na kutekeleza shughuli za VVU na UKIMWI kwenye maeneo
yao pamoja na kukuza mchango wa sekta ya umma na sekta binafsi katika mapambano
dhidi ya VVU na UKIMWI hapa nchini.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TACAIDS, Yasini Abasi alisema kuwa
uhitaji wa fedha za UKIMWI bado ni mkubwa kwani kwa sasa wafadhili wanaendelea
kupungua na hivyo kuitaka jamii kuendelea kuchangia mfuko wa udhamini wa
kudhibiti UKIMWI ili hata pale itakapo tokea waansitisha basi Mfuko uwe na fedha za kutosha kwa ajili ya huduma
za UKIMWI.
Kikao hicho kiliwashirikisha waratibu wa UKIMWI kutoka baadhi ya Wizarani,Halmashauri na Mikoa.
Waratib wa UKIMWI kutoka Wizarani, Halmashauri na Mikoa walioshiriki Kikao cha usambazaji wa taarifa ya mapitio ya
fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na sekta binafsi ya mwaka 2022
kilichoandaliwa na Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) wakiwa katika kikaohicho.
Mkuu wa MKoa wa Singida Peter
Serukamba (aliyekaa katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na Wawezeshaji wa zoezi la kukusanya taarifa za fedha za
UKIMWI kwenye sekta ya umma na sekta binafsi pamoja na waratibu wa UKIMWI
(aliyekaa kulia kwake) ni Mkurugenzi wa
fedha na Utawala wa TACAIDS, Yasin Abasi
na kushoto ni Mratibu wa wa UKIMWI MKoa wa Singida, Patrick Kasengo..
Picha hii imepigwa mara baada ya uzinduzi wa kikao cha usambazaji wa taarifa ya
mapitio ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na sekta binafsi ya mwaka 2022
Mkuu wa MKoa wa Singida, Peter Serukamba ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa
UKIMWI kutoka wizarani na baadhi ya
Waratibu wa Halmashauri nchini mara baada ya ufunguzi wa kikao cha uzinduzi wa
kikao cha usambazaji wa taarifa ya mapitio ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za
umma na sekta binafsi ya mwaka 2022 kilichofanyika leo Februari 20,2023 mkoani Singida. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa
Fedha na Utawala wa TACAIDS, Yasin Abasi na kushoto ni Mratibu wa UKIMWI Mkoa
wa Singida, Patrick Kasango.
Post A Comment: