Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Prof. Jamal Adam Katundu ( wa sita kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa taasisi zilizochini Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwemo OSHA kabla ya kuanza mbio za kimataifa za Kili Marathon Mkoani Kilimanjaro.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Prof. Jamal Adam Katundu (katikati) akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakikimbia mbio za Kili Marathon Km 21 Mkoani Kilimanjaro.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Prof. Jamal Adam Katundu (katikati) akimaliza mbio za Kili Marathon Km 21


Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa OSHA, Bi Netiwe Mhando (wakwaza kushoto) akikimbia mbio za Kili Marathon Kilomita 21


Baadhi ya watumishi wa OSHA ( katikati) wakikimbia mbio za Kili Marathon Km 5 Mkoani Kilimanjaro wakiambatana na taasisi zingine zilizochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

***********************

Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu na taasisi zake ikiwemo OSHA, wameshiriki katika mbio za Kimataifa za Kili Marathon Mkoani Kilimanjaro wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Adam Katundu katika mbio za Kilomita 21 na Kilomita 5.

Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu Bi. Edith Kisanji Simtengu amesema lengo kubwa la kushiriki katika mbio hizo ni kutekeleza sera ya kupambana na magonjwa sugu yasiyoyakuambukiza hivyo kuwafanya wafanyakazi wawe na afya njema na kuhamasika katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

“Tumekuwa tukishiriki mbio hizi za Kili Marathon mara kwa mara lakini awamu hii tumeona nivyema Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na taasisi zake tushiriki kwa pamoja ikiwa lengo ni kutekeleza sera yetu ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kujenga uhusiano mwema mahali pa kazi” Alisema Bi. Edith

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa OSHA, Bi Netiwe Mhando ambaye pia alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa mbio za Km 21 amesema kuwa ushiriki wa mbio hizo unatokana na majukumu ya msingi yanayosimamiwa na taasisi ya OSHA ikiwemo kuimarisha usalama na afya za wafanyakazi.

“Tunaposhiriki katika michezo kama hii maana yake tunahimiza wafanyakazi kujiweka katika hali nzuri ya kiafya hivyo kuilinda nguvu kazi ya taifa nashauri taasisi zingine kuhamasika katika kushiriki michezo na mazoezi mengine ili kuwasaidia wafanyakazi kujiweka imara, kuhamasisha ushirikiano na pia kuleta ari ya kufanya kazi katika maeneo yao ya kazi” alisema Bi Mhando.

Katika mbio hizo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Prof. Jamal Adam Katundu pamoja na watumishi wengine wa Ofisi ya Waziri Mkuu walifanikiwa kumaliza mbio za Km 21 huku watumishi wengine wakikimbia mbio za Km 5. Katika mwaka huu 2023 mbio hizi za Kili Marathon zinatimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002 zikikutanisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi katika mbio za kilometa 42, km21 na Km 5.

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: