Na John Walter-Manyara
Kuelekea Siku ya wanawake Duniani umoja wa polisi wanawake Mkoa wa Manyara (TPF NET MKOA WA MANYARA) wamekabidhi Taulo za kike Maboksi15 sawa na pisi 360 kwa wanafunzi wa Shule ya sekondari Komoto Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara.
Akizungumza na wanafunzi Mwenyekiti wa Polisi wanawake Mkoa wa Manyara SSP Georgina Matagi amewataka wanafunzi hao kujitambua pamoja na kuzingatia masomo na kuwaheshimu walimu pamoja na wazazi kwani wanamchango mkubwa katika masomo yao.
Aidha SSP Georgina ametoa elimu kwa wanafunzi hao juu ya namna ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia pamoja na madhara yake huku akiwataka watoto wa kike kutojiingiza katika mahusiano ili kuepuka mimba za utoni jambo litakalo sababisha kukatisha masomo yao.
Hatahivyo zaidi ya wanafunzi 1000 katika shule ya sekondari Komoto iliyopo Halmashauri mji wa Babati Mkoani Mwanyara wamefikiwa na elimu ya ukatili wa kijinsia na namna ya kukabiliana na ukatili huo ili kutimiza ndoto zao.
Ikumbukwe kuwa kila ifikapo tarehe 8 March kila Mwaka ni siku ya wanawake Duniani ambapo wanawake hutumia siku hiyo katika kudai pamoja na kupinga ukatili dhidi ya wanawake na kuenzi mchango mkubwa wa Mwanamke katika jamii.
Post A Comment: