Na;Elizabeth Paulo,Dodoma
Waziri wa Habari, Mawasiliano, na teknolojia ya Habari Nape Nnauye ametoa wito kwa waandishi wa habari kuendelea kuiamini serikali ya awamu ya sita kwamba mchakato wa kuwasilishwa kwa marekebisho ya sheria namba 12 ya mwaka 2016 ya Huduma za habari unaendelea.
Waziri Nnape ametoa wito huo leo alipokutana na waandishi wa habari jijini Dodoma mara baada ya kusikitishwa na kauli ya Jukwaa la wahariri Tanzania na kusema jambo hilo linakatisha tamaa kwa Serikali na kwa waandishi wa habari kuona Viongozi wanatoa kauli ambazo zinavunja moyo.
Nnape amesema muswada huo kwa mara ya kwanza utasomwa bungeni kwa mara ya kwanza February 10 .
“niseme kwa Masikitiko kwamba kauli ya jana ya jukwaa la wahariri inatusikitisha kama serikali kwasababu tumefanya kazi kwa muda mrefu katika mchakato wa mabadiliko ya sheria hii ya huduma za habari kwa pamoja tumekua na vikao vya usiku na mchana, tumepigiana simu usiku na mchana kuhakikisha tunafanya kazi pamoja sasa sikuelewa kwanini Jukwaa la wahariri walipanick na bahati mbaya wala hawakutaka ufafanuzi kutoka serikalini wakenda kutoa Statment ambayo ndani yake bahati mbaya kulikua na tuhuma kwanza zajumla kuwa serikali inadanadana kwenye mchakato huu wa mabadiliko ya sheria ya katiba.”Alisema Nape
Nape amesema Statment hiyo siyo ya kweli kwasababu tangu vikao kuanza serikali imekua ikifanya msukumo wa kuhakikisha mswada huo unawasilishwa.
“Mimi binafsi nimetoa muda wangu kukutana na kuzungunza na wadau kusukuma kupekeka taarifa sehemu tofauti tofauti hivyo jambo hilo limenisikitisha na ukisoma ile kauli ni kama vile serikali imegawanyika vipande vipande jambo ambalo siyo sahihi na mpaka nikawa nasikitika lengo la kauli hiyo ilikua nini kujaribu kuonyesha kama vile serikali tupo vipanda vipande”. Alisema
Amethibitisha kuwa Rais Samia na serikali yake ni moja na hakuna mgawanyiko wowote serikalini hivyo tuhuma za kusema kundi lingine linataka kundi lingine halitaki ndani ya serikali linapaswa kupuuzwa.
“Ukijaribu kusema hawa wanasukuma kulia hawa wanasukuma kushoto , hawa wanataka hawa hawataki tuhuma hizo siyo za kweli na zinapaswa nadhani kupuuza lakini kwenye ile kauli kuna vifungu vimewekwa vya kuonyesha kama vile vifungu havitakiwi na serikali.”Alisema Nape
Amesema serikali imemaliza kazi ya kufanya marekebisho ya ule mchakato na kwa makubaliano kifungu kwa kifungu na kusikitishwa na kuona yaliyoorodheshwa yalikua ndani ya makubaliano hivyo kwenda kuyatuhumu hadharani si jambo jema na zinavunja moyo hata kujenga chuki kwa wana habari kwa serikali jambo ambalo halipaswi kufanywa na Viongozi wahariri.
Amesema sheria hiyo hailengi kundi moja linalenga wanahabari wote na kwamba serikali ina nia njema ya kuhakikisha kwamba Sheria inapitiwa na kufika mahali pa makubaliano.
“Nitoe wito kwamba kweli tumesikitishwa na hili jambo kwahiyo endeeni kuwa na imani na mchakato huu kwamba utakwenda na utakwisha salama lakini tumefanya mengi pamoja kwa mashauriano na siyo kwenda kukimbia kusema hadharani kama kuna jambo halieleweke Milango iko wazi tuambizane . ” Alisisitiza Nape
Amesema Rais Samia anapaswa Kupchak shukrani kubwa kwa msukumo wa mchakato huo Mara baada ya kufanya kikao na waandishi wa habari ikulu Dar es salaam tarehe 28/6/2021 na kutoa maelekezo ya mchakato huo kuanza kwani miaka ya nyuma ilishindikana kabisa.
KAULI YA TEF
Februari 8, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) likisikika likisema limepokea kwa mshituko makubwa kauli ya Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa kuwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari (MSA 2016) umeshindikana kuingizwa bungeni kutokana na ripoti nyingi za Kamati za Kisekta za Bunge.
TEF imeona sababu iliyotolewa ni nyepesi na inapata wasiwasi iwapo kuna utashi wa kufanya mabadiliko katika sheria hii.
Aidha wamesema Katika vikao vilivyotangulia, waliona ugumu kutoka kwa baadhi ya maofisa wastaafu walioazimwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), maafisa kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,na baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama wakionesha wazi kutokuwa na nia ya kurekebisha sheria hii.
Wamesema Mara kadhaa vikao vilivyofanyika, viliisha bila mwafaka katika vifungu mbalimbali ikiwamo Mamlaka ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) chini ya vifungu vya 9 na 10, ambavyo vinampa mamlaka ya kuwa mlalamikaji, mwendesha mashitaka, mtoa hukumu na msimamizi wa utekelezaji wa hukumu;suala tunalosema ni ukiukwaji wa Utawala Bora na Utawala wa Sheria.
Post A Comment: