Na Elizabeth Joseph, Monduli.

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Monduli Mh,Isack Copriano pamoja na baadhi ya marafiki zake wamefanikiwa kugawa mbuzi 100 kwa Wazee 60 kutoka Kata ya Lemoot wilayani Monduli.

Awali Wazee hao kupitia kwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo waliomba kuwezeshwa kupata mradi utakaowawezesha kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kupatiwa mkopo na Halmashauri ya Monduli ambapo Mh, Copriano aliahidi kushirikiana na rafiki zake kutimiza ombi Hilo.

Mh, Copriano aliwataka Wazee hao kutumia mbuzi hao katika kufanikisha malengo yao ya kujikwamua ikiwa ni pamoja na kukifanya kikundi hiko kuwa cha mfano kwa wengine kutokana na mafanikio yatakayopatikana kupitia mbuzi hao.

Kwa upande wa mmoja wa Wazee hao Bw,Loshiru Paulo licha ya kushukuru kwa mradi huo waliopatiwa pia alieleza sababu ya kuomba mradi wa mbuzi kuwa ni pamoja na Wazee kutokumbukwa kwenye mikopo inayotolewa na Halmashauri na kushindwa kuendesha maisha yao ya kila hivyo kuamua kujiunga kikundi na kumuomba Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli kuwapatia mradi utakaowawezesha kujiendeleza.


Naye Diwani wa Kata ya Engutoto Nelson Lowassa alimpongeza Mwenyekiti huyo kwa kuwakumbuka wazee hao na kuongeza kusema jambo hilo linafaa kuigwa na baadhi ya viongozi wa siasa katika maeneo yao ili kusaidia wananchi wao.


Aidha katika ziara hiyo Mwenyekiti huyo aliweka jiwe la msingi katika Shule  Shikizi ya Msingi Ng’ambo na kuahidi kutatua changamoto zilizopo katika Shule hiyo ikiwemo ujenzi wa nyumba ya Mwalimu na ununuzi wa samani za ofisi kabla ya kufika 2025.





Share To:

Post A Comment: