Na Denis Chambi, Tanga.
SAID Kibula mwenye umri wa miaka 69 ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa 8 wa tukio la wizi wa mali mbalimbali katika ajali iliyotokea hivi karibuni wilayani Korogwe mkoani Tanga ikihusisha gari aina ya Fuso iliyogongana na Coaster iliyobeba mwili wa marehemu pamoja na waombolezaji wakitokea mkoani Dar es salaam kuelekea Moshi Kilimanjaro kwaajili ya mazishi amekutwa amejinyonga na Chandarua nyumbani kwake usiku wa february 22,2023 .
Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Tanga ACP David Chidindi amesema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Magira Gereza alikwa nje kwa dhamana ya mahakama ya hakimu mkazi Korogwe.
Itakumbukwa kuwa manamo February 3,2023 katika eneo la Magira Gereza tarafa ya Mombo wilayani Korogwe mkoani Tanga ilitokea ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu 17 na majeruhi 12 ambapo baadaye vifo viliongezeka na kufikia 21 wengi wao wakiwa ni wa familiya moja .
Wakati wa kuagwa kwa miili hiyo mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo aliibuka na kueleza namna alivyoshuhudia baadhi ya waokoaji walivyowaibia wahanga mali mbalimbali zikiwemo simu, nguo na fedha walizokuwa wamebeba .
Kufwatia ushuhuda huo serikali ilitoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwasaka watumiwa hao ambapo walifanikiwa kuwakamata watu 12 na kati yao 8 walikutwa na hatia.
Akieleza kuhusiana na tukio hilo mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba alisema kuwa mmoja kati ya watuhumiwa 8 aliyekutwa na nguo za marehemu zikiwa na damu usiku wa kuamia alhamis ya february 23 amekutwa amejinyonga nyumbani kwake , ambapo sasa wamebaki saba ambao wapo kwenye mkono wa sheria.
"Tulipata msiba wa ajali ya gari wiki kadhaa zilizopita lakini jambo la aibu lilitokea kwa majeruhi na marehemu kuibiwa vitu vyao na watu wote 12 tumewakamata na wanane kati yao baada ya uchunguzi ndio tuliwafikisha katika vyombo vya sheria na wapo mahakamani, na kwa bahati mbaya sana mmoja wapo ambaye tulimkamata akiwa na nguo za marehemu zikiwa na damu na mali nyinginezo ikiwemo simu za marehemu (jumatano) amejinyonga kwahiyo tumebaki na watu saba lakini wapo kwenye vyombo vya sheria.
Post A Comment: