Na Oscar Assenga,Tanga


Mkoa wa Tanga umezindua zoezi la ugawaji vyandarua kwa wanafunzi wa shule ya msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba kwa shule 1083.


Zoezi la ugawaji vyandarua hivyo limeratibiwa na serikali kupitia Wizara ya Afya na OR-TAMISEMI lengo ni kuhakikisha kiwango cha maambukizi ya malaria kinapungua hadi kufikia asilimia (0)ifikapo mwaka 2030


Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vyandarua hivyo kwa Wanafunzi,Mkuu wa mkoa wa Tanga Omar Mgumba amesema jumla ya vyandarua 529,641 vitagawiwa kwa wanafunzi katika shule zote 1083 za Msingi katika mkoa.

"Usambazaji wa vyandarua hivi mashuleni utatekelezwa kwa siku 45 na utaendelea katika Halmashauri za Korogwe,Muheza,Mkinga,Pangani,Handeni,Kilindi,Lushoto na Bumbuli"alisema RC Mgumba

Pia RC Mgumba amewataka vingozi wa serikali,dini na jamii kwa ujumla kusimamia matumizi ya vyandarua kwa usahihi vitakavyogawiwa kwa wanafunzi wa shule za msingi,na jamii ielimishwe juu ya matumizi sahihi ya vyandarua.

Naye Meneja wa MSD Mkoa wa Tanga,Sitti Abdulrahaman ameitaja mikoa itakayofaidika na vyandarua hivyo kuwa ni Iringa,Dodoma,Tanga,Manyara pamoja na Kilimanjaro.


"Lengo ni kupunguza maambukizi ya Malaria kutoka asilimia 7.5 kwa mwaka 2017 hadi kufikia kiwango cha chini cha asilimi 3.5 ifikapo mwaka 2025,na kutokomeza kabisa ifikapo mwaka 2030"alisema Meneja wa MSD Sitti.


"Bohari ya Dawa MSD ina majukumu manne ambayo ni uzalishaji,ununuzi,utunzaji na usambazaji wa bidhaa Afya,kwenda kwenye vituo vya afya ya Umma na vile vya binafsi zilizoidhinishwa na Wizara ya Afya,na imepewa jukumu la kusambaza vyandarua 529,641 vyenye thamani ya Shilingi Billioni 2.9 kwenye shule zote za msingi 1083 katika mkoa wa Tanga" alisema Meneja wa MSD Sitti.


Share To:

Post A Comment: