Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Walad Mwatawala akifungua mkutano huo, Kulia ni Mkuu wa Mradi wa GRILI Prof. Faith Mabiki.

Na Amina Hezron,  Njombe.

NAIBU Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Walad Mwatawala amepongeza Watafiti wa Mradi wa GRILI kwa kufanikiwa kufikia malengo yote matatu ya utafiti huo muhimu kwa Taifa.

Pongezi hizo amezitoa wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwisho wa Mradi huo unaofanyika Mkoani Njombe na kuwakutanisha wadau wote wa mradi kutoka ndani na nje ya nchi kupokea matokeo ya mwisho ya Mradi kutoka kwa wasimamizi wa Mradi huo na Wanafunzi waliokuwa wanasomeshwa na mradi  wakifanya tafiti mbalimbali.

“Sisi kama Chuo tumefurahishwa na utekelezaji wa mradi huu ambao ulikuwa na malengo makuu matatu ya kujenga uwezo na tutaona hapa waliyoyafanya, Kuzalisha  elimu mpya pamoja na mifumo mipya ya biashara kwenye eneo la mimea dawa ambayo ni muhimu kwa uchumi wa wadau kwenye mnyororo wa thamani wa mimea dawa nchini” alisema Prof. Mwatawala.

Aidha amesema kama Chuo wamefarijika kuona mradi umezalisha Wanafunzi watano (5) wa Shahada ya uzamivu kwenye masuala ya Mimea dawa na saba (7) wa shahada ya uzamili ambao kwa ujumla wameweza kuzalisha machapoisho ya kisayasi 17 kwenye eneo hilo muhimu huku akitumia nafasi hiyo kumpongeza Mkuu wa mradi huo Prof. Faith Mabiki kwa kazi kubwa aliyoifanya na wasimamizi wengine wa mradi huo ambao anaamini katika kipindi kifupi machapisho hayo ndiyo yamemuwezesha kupanda cheo kutoka Udaktari na kuwa Profesa.

Amesema mfumo mzuri wa biashara ya bidhaa za mimea dawa uliotengenezwa na Mradi huo utakuwa kichocheo kizuri cha mabadiliko na mafanikio ya biashara ya dawa asili kwakuwa anatambua dawa hizo zinauzwa kila kona nchini na watu wanazitumia lakini sasa kwa mfumo huu zitaweza kuuzwa katika mifumo rasmi.

“Kitu kingine muhimu ambacho ni kizuri mradi huu umefanya ni kuwaunganisha wadau wote kwenye mnyororo wa thamani wa bidhaa za mimea dawa kupitia Jukwaa lake la Ubunifu wa bidhaa zitokanazo na mimea dawa (GRIP) ambalo limesaidia kuwaweka pamoja wadau wote na kujadiliana maendeleo na changamoto na kuzitatua kwa pamoja ambalo linasimamiwa na SUA lakini wazo lilitoka kwenye mradi huu wa GRILI” alipongeza Prof. Mwatawala.

Akizungumza malengo na mafanikio ya Utafiti Mkuu wa Mradi huo Prof. Faith Mabiki amesema mradi ulijikita katika kushughulika na bidhaa zitokanazo na mimea dawa kwa maana ya tiba asili na mnyororo mzima wa thamani ili kusaidia Tanzania kunufaika na utajiri mkubwa ilionao wa maliasili hususani mimea dawa  kwa kufikia soko la Dunia.

Aidha amesema utafiti huo ulilenga kusaidia Tanzania kufikia mpango wake wa maendeleo endelevu wa 2025 unaotambua mchango wa matumizi ya maliasili ikiweo mimea dawa ambayo ipo nchini na inatumiwa lakini haijaweza kushika vyema Soko la ndani na kimataifa na kuchangia maendeleo ya wadau wa tiba asili.

Amesema changamoto kubwa iliyoletwa na Tafiti zinazofanywa na mradi huo ni namna ambavyo sasa wanaweza wakachukua matokeo ya mradi huo ili kuyakuza kuleta maendeleo ya wadau binafsi katika kuongeza ubora na Masoko.

 Prof. Mabiki amesema jambo lingine kubwa ambalo kama Chuo wanajivunia na kufanikiwa kupata kifaa cha kisasa cha kupima kemikali za mimea dawa, Madawa na vyakula ambacho kitaendeea kusaidia Watafiti, Wanafunzi na wadau wengine kukikutumia katika kufanya tafiti mbalimbali hapahapa nchini.

Mradi wa GRILI-DANIDA unatekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine(SUA) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Chuo Kikuu cha Sayansi na teknolojia Afrika cha Nelson Mandela (NM-AIST), Chuo Kikuu cha Mzumbe, Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda Tanzania(TIRDO), Taasisi ya taifa ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu, NIMR, Chuo kikuu cha Copenhagen cha nchini Denmark kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Denmark DANIDA.

Mtafiti Mkuu wa Mradi wa GRILI Prof. Faith Mabiki akiwasilisha malengo na mafanikio ya Mradi huo. 
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Jeremy Kusiluka akitambulisha washiriki na ratiba ya siku hiyo ya kwanza ya mkutano huo.
Picha ya pamoja ya Washirika wa Mradi Mkutano huo kutoka taasisi mbalimbali nchini na kutoka nje ya Tanzania.
Mkutano ukiendelea.
  Washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia mawasilisho ya tafiti mbalimbali zilizofanywa na mradi huo kupitia Wanafunzi wa Shahada ya Uzamivu na Uzamili.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea
Mkutano ukiendelea.


Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: