Kauli hiyo imetolewa Hii Leo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Ndugu Moitiko Kisioki , Wilayani Monduli Mkoani Arusha katika ziara yake ilioanza Leo katika kata ya Loorkisale na Lemooti Wakiongozana na kamati ya utekelezaji Wilaya.
Awali akizungumza na Wanachama na jumuiya wa kata ya Loorkisale Ndugu kisioki baada ya kusikiliza taarifa fupi iliwasilishwa Moja ya maombi yaliombwa ni kuwezeshwa kupatikana Kwa kitega uchumi (viti 200) ,Kwa ajili ya kukodisha ambapo Kisioki amepokea na kuahidi viti hivyo mwezi wa nne mwaka huu .
Wakati huohuo katika kata ya LEMOOTI, amepokea ombi la Wazee kuwezeshwa ambao wao waliomba mradi wa mbuzi ambapo jumla ya mbuzi waliopatikana ni ishirini(20) kutoka Kwa wadau / kamati iliyoongozana na mwenyekiti , huku ndugu Kisioki akitoa mbuzi 35 Ambapo jumla yake ni Mbuzi dume 55.
" Nimeona nianze na wazee wangu hapa kama mlivyoniomba na hii ni kwa sababu mmesema mmesahaulika si kama wamama na vijana ambao wao wanapatiwa mikopo na Wana asilimia Yao halmashauri ,tengenezeni zizi vizuri na hata viongozi wengine walioahidi wilayani wakumbusheni ahadi zao". Amesema kisioki
" Lakini mbali TU na wazee mimi nimekuwa nikiwasaidia sana vikundi vya kina mama , hapa Lemooti Kuna vikundi 23 kama sio zaidi sitaki kuahidi kitu lakini omba nilichukue hili NAMI nikatafuta la kufanya baada ya wiki hivi nitakuja na Millioni kumi na Moja na laki tano 11,500,000 lakini natoa kazi kila kikundi na chenyewe kiandae laki tano ili nikikupa nawe unaweka million zako Tano kama huna nami Sina ili tuweze kufanya mradi wenye tija tukutane site". Amesema kisioki.
Kwa upande wake katibu wa Jumuiya hiyo Bi . Bitrice Mandia amesema lengo la ziara ni kushukuru wanachama na jumuiya Kwa ushindi, Kukagua uhai wa Chama na Jumuiya zake huku akisisitiza kufanyika kwa vikao mara Kwa mara na kutaka mukhatasari wa Kila kikao kufikishwa ofisini kwake.
Bi. Bitrice ameongeza kwa kusema kuwa kazi kubwa ya Jumuiya ya wazazi Ni malezi na hivyo ametoa Rai kwa wazazi kujijengea urafiki na watoto wao na utaratibu wa kuwakagau watoto pindi wanaporudi mashuleni au machungani kwani kumeibuka tabia ya watoto kulawitiana wenyewe.
Ni siku ya kwanza ya ziara ya mwemyekiti wa jumuiya ya wazazi Ndugu kisioki Wilayani Monduli katika kata Lorkisale na Lemooti ambapo hapo kesho ataendelea na ziara Yake Kwa kata zote 20 wilayani humo ,Kwa lengo la kushukuru ,kukagua Uhai wa Chama na Jumuiya zake pamoja na kutoa Elimu Kwa viongozi waliochaguliwa kujua Majukumu Yao.
Post A Comment: