Na John Walter-Babati

Wananchi wilayani Babati mkoani Manyara,  wametakiwa kuboresha mazingira kwa kuhakikisha wanapanda miti kwa wingi.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange wakati wa zoezi la upandaji  miti katika kituo cha afya Maisaka mjini Babati ambapo amesema katika wilaya ya Babati atahakikisha zoezi hilo linafanyika kikamlifu.

Amesema agizo hilo la serikali kupitia ofisi ya makamu wa Rais kupandwa miti milioni 1.5 kila Halmashauri, katika wilaya ya Babati atatumia mbinu mbalimbali za uhamasishaji ili lengo litimie.

Aidha amewataka wananchi kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda miti ya matunda na vivuli ili kulinda na kutunza mazingira.

Twange amesema mbali na miti kupandwa katika maeneo ya taasisi kama Shule, Hospitali, Zahanati na vituo vya Afya, lakini pia kampeni ya upandaji miti itawafikia wanachi wote kwa kugawa miti kwa kila mwananchi kupitia watendaji kwenye mitaa na vijiji.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Abdulrahmani Kololi (Diwani wa Maisaka) amesema watahakikisha katika halmashauri hiyo kila mwananchi anapanda mti.

Kiongozi wa Walimbwende  mkoa wa Manyara Aminatha ambaye ameshiriki pamoja na walimbwende walioshinda Miss Tanzanite 2022, amewaasa warembo kujiutokeza kushiriki kupanda miti katika maeneo yao.


Share To:

Post A Comment: