WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na teknolojia Prof.Adolf Mkenda amekemea vikali tabia ya wizi na kughushi mitihani unaofanywa na baadhi ya walimu na shule na kusema walimu wote wanaobainika kufanya wizi huo wafukuzwe kazi na kufunguliwa mashtaka.


Aidha amewaasa wazazi na walezi kusimamia suala la maadili na malezi kwa watoto ili kupunguza wimbi la watoto kuiga mambo ya utandawazi zaidi hali inayosababisha kushuka kwa maadili na malezi yanayoendana na Taifa letu.

Akizungumza na watumishi,na mameneja wanaosimamia vitengo mbalimbali vinavyoendesha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa elimu ADEM Bagamoyo Mkoani Pwani ,Mkenda alieleza ,hali ya mtihani ni nzuri nchini ila wale wachache ambao wanaendelea na wizi Wizara imejipanga kukomesha na kuwatia adabu.

"Hali ya mitihani nzuri sana ,ila tukicheza na hawa wachache itatokea mlipuko kwa kuotesha mizizi"usipojenga ufa utajenga ukuta"

"Nimesikitika sana kuona wapo walimu wa aina hii,Walimu wote waliohusika na wizi wafukuzwe kazi na sheria iwe na meno kuwabana wamiliki wa shule na walimu wa aina hii"

"Unakuta mtoto anabidii ya kusoma ,ili afaulu mitihani yake, haiwezekani mwingine abebwe kwa kutumia jitihada za mwenzie ,Tukizungumzia malezi na maadili sio tuu ya tamaduni ,Mila na desturi,hata hili ni malezi mabaya kumfundisha mtoto kufanya wizi wa mitihani"alifafanua Mkenda.

Vilevile Mkenda, alisema changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya ADEM inafahamika ,suala la kufanyiwa ukarabati linafanyiwa kazi.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ADEM mtendaji Mkuu wa ADEM ,Siston Masanja alieleza ipo changamoto ya kuwepo kwa majengo ya kale ambayo yanatakiwa kufanyiwa ukarabati.

Changamoto nyingine ni wakurugenzi wa Halmashauri kusita kutoa watumishi wao kwenda kupata mafunzo ADEM.

Siston alieleza pia wamekuwa washauri kuanzisha Taasisi kama ADEM Zambia,Malawi,Afrika Kusini na Kenya ambayo imepiga hatua zaidi.

Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wakala umepanga kudahili walimu 2,343,katika kozi za CELMA,DEMA na DSQA,kutoa mafunzo ya uongozi na usimamizi wa shule kwa walimu wakuu 17,000,kutoa mafunzo ya utawala bora kwa wasimamizi wa elimu katika Mamlaka za Serikali za mitaa 6,432.

Kuanza ujenzi wa kampasi ya ADEM Mwanza,na kuanza ujenzi wa jengo la mihadhara katika kampasi ya Bagamoyo lenye uwezo wa kuchukua walimu 1,000.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Halima Okash alieleza Serikali inaendelea kushirikiana na wadau,jamii , Taasisi mbalimbali kuboresha Mazingira ya sekta ya elimu.


Share To:

Post A Comment: