Wizara ya Maji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (Mbeya-UWSSA) imesaini mkataba wenye thamani ya shilingi Bilioni 117.5 na mkandarasi kampuni ya China Railway Construction Engeneering Group kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka chanzo cha maji cha mto Kiwira. Mradi huo unatarajia kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji katika jiji la Mbeya kutoka lita milioni 66.5 zinazozalishwa kwa siku hadi lita milioni 184 kwa siku.


Akizungumza jijini Mbeya katika hafla ya utiaji saini mkataba huo Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema fedha zote za utekelezaji wa mradi huo zimetolewa na serikali. Amesema Wizara ya Maji imejipanga kuhakikisha fursa ya vyanzo vya uhakika vya maji inatumika kuondoa changamoto ya majisafi sehemu mbalimbali nchini.



Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Ujenzi na Ufuatiliaji Miradi Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amesema awamu ya kwanza ya utekekezaji wa mradi huo itakamilika katika kipindi cha miaka miwili kuanzia Februari 25 mwaka huu hadi Februari 24, 2025.



Naye Mbunge wa Mkoa wa Mbeya kupitia Viti Maalum Wanawake Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wa Mbeya wanapata maji ya uhakika kupitia chanzo hicho.


Amewahakikishia wananchi wa mbeya kuwa serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia ni sikivu, itahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati ili akinamama wa Mbeya waondokane na changamoto ya huduma ya majisafi na salama.




Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: