Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akiongea na waandishi wa habari wa Iringa juu ya kiasi cha fedha kinachohitajika kukamilisha ujenzi wa machinjio ya kisasa ya Ngelewala
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akiongea na waandishi wa habari wa Iringa juu ya kiasi cha fedha kinachohitajika kukamilisha ujenzi wa machinjio ya kisasa ya Ngelewala
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada amesema kiasi cha shilingi bilioni 1.9 kinaitajika ili kukamilisha ujenzi wa machinjio ya kisasa ya Ngelewala ili ianze kutoa huduma ya uchinjaji wa nyama kwa kisasa.
Akizungumza wakati wa ziara ya waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda, Ngwada alisema kuwa machinjio hiyo imetumia zaidi ya bilioni 2 katika ujenzi wake hadi ilipofikia na imeanza kufanya kazi.
Ngwada alimuomba waziri mstaafu Mizengo Pinda kuwasaidia kupata kiasi cha shilingi bilioni 1.9 ambazo wanauhakika zitamalizia ujenzi wa machinjio hiyo ya kisasa iliyopo katika Manispaa ya Iringa.
Alisema kuwa kukamilika kwa machinjio hiyo ya Ngelewala kutaongeza ajira ya zaidi ya watu 400, kukuza mapato ya Manispaa ya Iringa na kukuza uchumi wa wananchi wote wa Halmashauri ya Manispaa hiyo.
Meya Ibrahim Ngwada alimazia kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya mradi huo wa machinjio ya kisasa ya Ngelewala.
Kwa upande wake waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda alisema kuwa amejionea hatua iliyofikia machinjio ya kisasa ya Ngelewala hivyo ataenda kuongea na viongozi wa ngazi za juu kuhakikisha fesha zilizobaki za kiasi cha shilingi bilioni 1.9 zinapatika na kumalizia ujenzi wa machinjio hiyo.
Pinda alisema kuwa kukamilika kwa machinjio hiyo ya kisasa Kutachochea kasi ya kukua kwa uchumi wa wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Halmashauri nyingine.
Post A Comment: