Na John Walter-Babati
Mbunge wa Babati Vijijini Daniel Sillo amesema Daraja la Gichameda kata ya Magugu lililogharimu Shilingi Bilioni 1,191,915,000 limekamilika na limeanza kutumika.
Kukamilika kwa daraja hilo linalounganisha Gichameda na vijiji vingine vya kata ya Magugu, kunatoa fursa kwa Wananchi kuweza kusafirisha mazao yao kwa urahisi.
Sillo amewataka Wananchi kuonesha uchungu kwenye kodi zao kwa kulitunza daraja hilo ili lidumu kwa muda mrefu.
Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo ambazo zimewezesha ujenzi wa daraja hilo.
Akielezea mchanganuo wa fedha hizo Meneja wa TARURA wilaya ya Babati Mhandisi Aloyce Nombo, amesema Gravel yenye ukubwa wa km 9.3 shilingi milioni 168,021,500, kuchonga km 9.3 shilingi milioni 20,460,000, kunyanya tuta km 1.8 shilingi milioni 221,000,000, Pipe Culvert 19 kwa shilingi 114,000,000, River training km 2 sawa na shilingi 167,750,000, ukuta wa mawe kuzuia maji shilingi 97,500,000, daraja mita 22 shilingi 360,283,500 pamoja na gharama za awali shilingi milioni 43,400,000 ambazo jumla yake ni shilingi Bilioni 1,191,915,000.
Wananchi wa Kijiji cha Gichameda wamemshukuru Mbunge na serikali kwa kuharakisha ujenzi wa daraja hilo ambalo ni kiunganishi Muhimu na vijiji viingine.
Wanasema awali walikuwa wakiteseka kusafirisha mazao yao na kufuata huduma zingine za kijamii zikiwemo za Afya.
Katibu wa chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Babati Filbert Mdaki amempongeza Mbunge huyo kwa jitihada zake za kuwasemea wananchi bungeni na hatimaye daraja limepatikana.
Diwani wa kata ya Kisangaji Adamu Ipingika amesema daraja hilo lilikwamisha maendeleo kwa muda mrefu lakini kupitia Rais Samia na Mbunge wa Sillo fedha zimepatikana na daraja limejengwa.
TARURA Babati Vijiji wamesema awali walikuwa na shilingi milioni 200 tu lakini Mbunge huyo amefanikisha pesa zaidi kupatikana na kukamilisha daraja hilo.
Post A Comment: