Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida , Yagi Kiaratu akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani  kilichoketi leo Februari 1, 2023 kwa ajili ya mapitio ya utekelezaji wa mpango na bajeti.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MANISPAA ya Singida inatarajia kukusanya na kutumia Sh. Bilioni 33.607  katika mwaka wa  fedha wa 2023/ 2024.

Hayo yalibainishwa na Afisa Mipango wa halmashauri hiyo, Selestine Masawe katika kikao cha baraza la madiwani kilichoketi kwa ajili ya mapitio ya utekelezaji wa mpango na bajeti.

Masawe alisema makadirio yamezingatia mwendo halisi wa hali ya kiuchumi nchini na duniani ukusanyaji wa mapato ya ndani na jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na halmashauri hiyo za kuongeza mapato.

" Makadirio haya yamezingatia mahitaji yasiyoepukika kama vile kugharamia miradi mbalimbali, madeni ya halmashauri na mishahara ya watumishi wa umma" alisema Masawe.

Masawe alisema matumizi ya kawaida ni Sh.Bilioni 3.859, ambapo mapato ya ndani ya ndani ni Sh.Bilioni 3.103, ruzuku Sh.Milioni Milioni 756.158.

Alisema miradi ya maendeleo ni Sh.Bilioni 10.277, ambapo mapato ya ni Sh.Bilioni 7.650 na ruzuku ni Sh.Bilioni 7.650 na kuwa makadirio ya bajeti ya mishahara ni Sh. Bilioni 19.469 sawa na asilimia 58 ya bajeti ya halmashauri.

Akizungumzia mapato na matumizi ya ya bajeti ya mwaka 2021/ 2022 alisema halmashauri ilikadiria kukusanya na kutumia Sh.Bilioni 35.548  na hadi Juni 2022 ilikusanya jumla ya Sh.Bilioni 29.476.

Alisema kiasi hicho kinajumuisha Sh. Bilioni 4.805 mapato ya ndani ya lengo la mwaka la Sh.Bilioni 29.911 na kuwa halmashauri ilitumia Sh.Bilioni 28.551 kugharamia utekelezaji wa shughuli na miradi mbalimbali ya halmashauri.

Alisema kati ya kiasi hicho, Sh.Bilioni 21.423 ni matumizi ya kawaida na Sh.Bilioni 7.127 ni matumizi ya maendeleo.

Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye ni Mstahiki Meya, Yagi Kiaratu alisema wataongeza nguvu ya kukusanya mapato na kupunguza matumizi yasio ya lazima ili fedha zitakazopatikana zielekezwe kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi hivyo sisi madiwani ndio wenye wajibu wa kusimamia matumizi ya fedha hizo wakati wa utekelezaji wa miradi hiyoili ilingane na thamani halisi ya fedha zilizotolewa" alisema Kiaratu.  

Kikao hicho kikiendelea. Kutoka kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Hassan Mkata, Mstahiki Meya, Yagi Kiaratu na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Jeshi Lupembe.
Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Hassan Mkata, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
 Afisa Mipango wa halmashauri hiyo, Selestine Masawe akiwasilisha mpango wa bajeti ya 2023/2024 katika kikao cha baraza la madiwani kilichoketi kwa ajili ya mapitio ya utekelezaji wa mpango na bajeti.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida, Lucia Mwiru, akizungumza  kwenye kikao hicho
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.

 Kikao kikiendelea. 


Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: