Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akiongea wakati wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuhusu rasimu ya bajeti ya 2023/2024

Na Fredy Mgunda, Iringa.




BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Iringa limeazimia kupitisha vyanzo vyote vya mapato vinavyopatikana katika halmashauri ili kuongeza mapato kufikia billion 10 tofauti na matazamio ya miaka ya nyuma ya kukusanya shilingi billion 4.

Hayo yamezungumzwa na Meya wa manispaa ya Iringa Mh.Ibrahimu Ngwada ambapo amesema kuwa nia ya miaka mitatu iliyobakia katika baraza hilo ni kufikia mapato ya shillingi billioni 6 mapato ambayo yatapatikana kutoka katika kata mbalimbali.

“Hili Ni baraza la kupokea  taarifa na kupitia vyanzo vya mapato katika kila kata halmashauri yetu mkakati wetu ulikuwa ni kukusanya shillingi billioni 3.5 hadi billioni nne lakini sasa kupitia vyanzo hivi mpaka miaka mitatu hii ya baraza kukamilika tunatarajia kufikisha billioni 6 kutoka billioni 3.5 

“Alisema kuwa endapo mapato yatasimamiwa vizuri yatasaidia kutatua baadhi ya changamoto zilizopo katika kata mbalimbali na hivyo kurahisisha utenda kazi 

“Mapato hayo yakiongezeka yatakuwa msaada katika kuongeza vituo vya afya ,kuboresha miundombinu ,masoko yetu yatakuwa vizuri na pia haya mapato yatasaidia kuongeza nguvu kwenye mikopo ya halmashauri ile ya asilimia 10  kwa hivyo tutazame vizuri namna ya kuona kwa uzuri haya mapato katika kila kata" alisema Ngwada

Aidha Ngwada Katika hatua nyingine alisema kuwa pamoja n akutazama vyanzo vya mapato violivyopo katika kata wametizamia uwepo wa minara ambayo imekuwa ikiingiza mapato makubwa kwa kwa wamiliki binafsi wa minara hiyo nje na Halmashauri kufaidika na mapato yanayopatikana katika minara kikao hicho maalumu cha kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato katika halsmashauri kimehairishwa na naibu meya manispaa ya iringa mh.jully sawani mpaka watakapokutana tena

 "kwanza niwapongeze watendaji kwa kuwaisilisha taarifa za kata vizuri mapato ya halmasahuri yetu jukumu letu ni kusimamia hiyo nia ili tuweze kusonga mbele lakini pia kiutaratibu baraza letu yapo mengi yaliyojadiliwa hapa yanaweza kujadiliwa kwenye vikao vyetu tena kwa hiyo bajeti yetuitaelekeza mambo ya ujumla tunayonafasi pia ya kwenda kuhakikisha halmashauri yetu inakwenda mbele"

Kwa upande wao madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamepitisha vyanzo vya mapato na kuwataka wataalamu kurudi wakiwa na majibu na mipango thabiti katika kikao kijacho ili kuliweka vizuri suala la mapato ya minara  pamoja na kuwataka  afisa biashara,mchumi, na mwanasheria kutembelea baadhi ya halsmashauri ili kuona namna wanavyopata mapato kupitia minara na vyanzo vingine mbalimbali.

Katika hatua nyingine naibu Meya July Sawani amesem akuwa uwepo wa madiwani katika halmashauri ni kuhakikisha mapato na matumizi yanafanyika vizuri huku akiwataka watendaji wa serikali na mkurugenzi kuongeza vyanzo ambavyo wanafikiri vitasaidia kuongeza tija katika halmashauri 

“Pia tunamuelekeza mkurugenzi pamoja na wataalamu vyanzo ambavyo mnafikiri vitasaidia halmashauri lakini vyanzo pia ambavyo tunafikiri haviko sahihi vitajionesha kwenye bajeti vyote wala msiwe na shaka kesho vitajionesha tuweze kuweka vizuri halmashauri yetu ili tusonge mbele nia ya serikali ya kuweka madiwani ni kuhakikisha wanaishauri halmashauri mapato yanakuwa sahihi pia matumizi yake yanafanya kazi iliyokusudiwa"

 
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: