Na;Elizabeth Paulo ;Dodoma
Serikali katika kulinda usalama wa bahari kuu wameweka mifumo ya kulinda usalama kushirikiana na Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu
ikiwa ni pamoja na kutumia mifumo ya kufuatilia meli ndani ya maji na kutumia doria za ndege kwa ajili ya kuangalia kinachofanyika.
Hayo yameelezwa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt.Emmanuel Sweke alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maendeleo ya mamlaka hiyo tangu kunzishwa kwake kisheria mnamo mwaka 2010.
Dkt.Sweke amesema maendeleo ya mapato ndani ya bahari kuu ambapo amesema tayari mwekezaji kutoka nchini hispania anatarajia kujenga kiwanda cha kuchakata samaki ambacho kitajengwa katika bandari ya Tanga .
Amesema kuwa mpaka kiwanda hicho kikamilike kitagharimu kiasi cha dola milioni 10,kitazalisha ajira kwa watanzania 100 na kinatarajiwa kuchakata takribani tani 200 kwa siku.
Kadhalika Dkt.Sweke amesema kuwa pamoja na Uvuvi kuwa ni gharama kubwa lakini umeweza kuliingizia pato taifa kwa njia za utoaji leseni kwa meli za ndani na nje ambazo zinataka kufanya biashara ya uvuvi katika bahari kuu.
Ambapo amesema mwaka 2010 walitoa leseni kwa meli za uvuvi 536 na mwaka 2015 walitoa leseni kwa meli za uvuvi 596.
“Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu umekuwa na majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoaji wa leseni kwa meli ambazo zinatakiwa kufanya uvuvi na kuhakikisha zinapokuwa zimepewa leseni zinakuwa na bendera ya Tanzania,
“Pamoja na kuwa na bendera ya Tanzania lazima kuwepo na usimanizi wa kulinda usalama wa wavuvi na meli zao kwa kuhakikisha hakuna uvuvi haramu ambao umekuwa ukijitokeza katika bahari hiyo”ameeleza Dkt.Sweke.
Mamlaka hiyo katika kipindi cha mwaka 2022 hadi kufikia wiki mbili zilizopita uvuvi wa bahari kuu umeingiza pato la taifa kiasi cha sh.bilioni 4.1 kwa shughuli za utoaji wa leseni kwa meli za uvuvi.
Post A Comment: