Mkurugenzi wa sera na mipango wizara ya Afya Bw.Edward Mbaga amefungua rasmi kongamano la kimataifa la madaktari Bingwa wa ubongo Mgongo na mishipa ya fahamu ulilojikita kwenye matibabu na uchunguzi wa uvimbe kwenye ubongo, mgongo pamoja na saratani ambapo zaidi ya madaktari bingwa 200 kutoka mataifa mbalimbali wanashiriki.
Bw. Mbanga amesema pamoja na maboresho makubwa kwenye sekta ya afya hapa nchini Serikali inampango wa kuongeza watalam wa fani ya upasuaji na ubongo kutoka 100 hadi 250 katika kipindi cha miaka 10.
Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini MOI Prof. Charles Mkony amesema kongamano la mwaka huu limelenga kuwapa wataalam hapa nchini mbinu za kisasa za uchunguzi na matibabu ya uvimbe kwenye ubongo na mgongo uliombatana na saratani.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt.Respicious Boniface amesema takwimu zinaonyesha zaidi ya wagonjwa 1724 wamepokelewa wakiwa na uvimbe kwenye ubongo ulioambatana na saratani katika kipindi cha miaka 5.
“Mafunzo yatahusisha nadharia na vitendo kwa siku tano ambapo wagonjwa Kati ya 5-10 watafanyiwa upasuaji kwa mbinu za kisasa” Alisema Dkt. Boniface
Mkufunzi kutoka chuo kikuu cha Coronado (USA) Prof. Ryan Ormond ameushukuru uongozi wa MOI kuendeleza Uhusiano kati ya MOI na Chuo kikuu cha Colorado ambapo madaktari na wagonjwa wanufaika.
Post A Comment: