Mganga mkuu wa mkoa wa Tanga Japhet Simeo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma zitakazotolewa kwa siku tano na madaktari bingwa kutoka Hospital ya Benjamini Mkapa.
Na ,Denis Chambi, Tanga.\
JOPO la madaktari 12 wakiwemo madaktari bingwa 9 wa magonjwa ya upasuaji kutoka hospital ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma wameweka kambi ya siku tano mfululizo katika Hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo kwaajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa zaidi 200 wenye matatizo mbalimbali ikiwemo mishipa ya fahamu, mifupa , mfumo wa haja ndogo na magonjwa ya uzazi wa kwa akina mama.
Aidha madaktari hao watatoa pia huduma kwa wagonjwa wenye matatizo ya magonjwa ya ndani , tiba ya moyo kwa watoto na watu wazima, magonjwa ya watoto, magonjwa ya macho pamoja tiba ya kinywa na meno.
Akizungumza mkurugenzi msaidizi wa hospital ya Benjamini Mkapa ambaye pia ni daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu Henry Humba alisema kuwa kuna uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali kupitia wizara ya afya katika kuboresha huduma ambazo awali ilikuwa inamlazimu mgonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi ambapo sasa hapa nchini huduma hizo zinapatikana hii ikienda sambamba na kuwasomesha wataalam mbalimbali ambao sasa wamekuwa wakihudumia wananchi wenye matatizo mbalimbali.
"Hizi ni huduma ambazo miaka iliyopita zilikuwa zinapatikana nje tu au hospital moja hapa nchini lakini sasa huduma hizi zipo hata katika hospital za kanda za rufaa kwahiyo ni uwekezaji mkubwa , na kwa Benjamin Mkapa kuna huduma nyingi sana ambazo zimeanzishwa na serikali ikiwemo maabara ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo na upasuaji ambapo huduma hii ilikuwa tu pale Muhimbili "alisema Dkt Humba.
" Tumejiandaa pamoja na kuona wagonjwa wa nje lakini kwa wale ambao wanafanyiwa upasuaji wale ambao kutakuwa na uwezekano wa kuwafanyia upasuaji ambapo utakuwa salama kufanyika kayika maeneo ya hospital tunawafanyia hapa hapa"
Alisema licha ya kuhudumia wagonjwa Watakaofika katika kambi hiyo wanatarajia pia kutoa uzoefu kwa madakatari waliopo katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo pamoja na kutoa elimu kwa wananchi namna wanavyoweza kuchukua tahadhari ya kujikinga na magonjwa mbalimbali.
" Moja wapo ya malengo ni kitoa uzoefu kwa madaktari wetu kutokana na uwekezaji mkubwa ambao umeshakwishakufanywa na serikali katika hospital hizi za mkoa tunajua kuna vyumba vya wagonjwa mahututi, CT Scan kwahiyo huu ni muda ambao tutautumia na sisi kubadilishana uzoefu wa kielimu kwa wenzetu"
Aidha aliongeza kuwa sasa hivi magonjwa ambayo sio ya kuambukiza yamekuwa ni tishio kwa jamii na wagonjwa wamekuwa wakiongezeka mara kwa mara.
"Matatizo kwa mfano ya moyo yako mengi sana na magonjwa ambayo yanatishia sasa hivi ni magonjwa ambayo sio ya kuambukiza kama vile ajali lakini huduma hizi zipo kutokana na uwekezaji uliofanywa na serikali na kadiri uwekezaji unavyofanjwa ndivyo ubainishaji wa haya magonjwa unavyoongezeka na tafiti bado zinaendelea lakini wagonjwa wapo kwa kiasi kikubwa" alisema Humba.
Mganga mkuu wa mkoa wa Tanga Japhet Simeo alisema kuwa ujio wa wataalam hao utakuwa na tija kwa madaktari waliopo katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo wakitarajia kupata uzoefu wa kitabibu .
"Kwa hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo tunaona watumishi wetu watakavyokwenda kunufaika kwa kupata sehemu ya taaluma ambazo madaktari bingwa hawa watakuwa wakizitumia katik kutibu maana yake tuntarajia tutavuna utaalamu kwa madaktari wetu wa kawaida na madaktari bingwa" alisema Simeo.
Simeo aliwataka wananchi wa mkoa wa Tanga jujitokeza kwa wingi kuatiwa matababu hayo kwa wale ambao watabainika ambapo a kambi hiyo ambayo inaanza February 27 hadi march 3, 2023 ikifanyika kwa muda siku tano na kwa wagonjwa ambao hawana bima ya afya watapata huduma kwa gharama nafuu.
Post A Comment: