Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akimkabidhi ofisi mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica kessy na kumueleza changamoto ambazo anatakiwa kuzifanyia kazi.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akimkabidhi ofisi mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica kessy


Na Fredy Mgunda, Iringa.


MACHINJIO ya kiasasa yageuka kaa la Moto kwa viongozi wa serikali ya wilaya ya Iringa kuwa machinjio hiyo ilianza kujengwa mwaka 2008 hadi hivi Sasa bado haijakamilika ikiwa imetumia zaidi ya shilingi bilioni mbili  kwa ujenzi na inauwezo wa kuchinja ng'ombe mia moja(100), Mbuzi mia mbili(200) kwa siku

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo wakati akikabidhi rasmi Ofisi kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Veronica Kessy kumuomba aishughulikie Changamoto ya kutokamilika kwa wakati machinjio ya kisasa ya Ngelewala.

Moyo akikabidhi ofisi pamoja na miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Iringa alisema Mchinjio hivyo inayotia dosari utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuwa imetumia zaidi ya Miaka nane tangu ilipoanza kujengwa hadi sasa haijakamilika.

Alimuhimiza Mkuu wa Wilaya ya Iringa kuhakikisha anawabana Maafisa wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wanasimamia Mradi huo ili kuongeza msukumo wa uwajibikaji utakaofanikisha kukamilishwa Kwa Mradi huo ambao ni sehemu ya miradi itakayoongeza mapato ya Halmashauri hiyo pamoja na kutanua soko la ajira Kwa wafanyabiasha mbalimbali wakiwemo wanajihusisha na biashara ya kitoweo.

Moyo aliwaomba Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Watumishi wa Halmashauri zote za Wilayani humo pamoja na Wananchi kumpa ushirikiano mkuu wa Wilaya ya Iringa  Veronica Kessy akieleza kuwa mafaniko aliyoyapata kwa kipindi alichokaa Iringa ni matunda ya ushirikiano waliompatia hivyo ni muhimu wakaendeleza ushirikiano huo Kwa mkuu huyo wa Wilaya.

"Kwa kweli Sina neno zaidi ya kuwashukuru, Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Watumishi wa Halmashauri zote, Viongozi wa Chama Cha mapinduzi CCM pamoja na Wananchi hakika nimefanyakazi nanyi Kwa mafanikio, niwaombe ushirikiano mlionipa muuendeleze pia Kwa mkuu wenu wa Wilaya wa Sasa ambaye nimemkabidhi kijiti" Alisema Mohamed Hassan Moyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Veronica Kessy mara baada ya kukabidhiwa ofisi ameahidi kuendeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake na kusisitiza ushirikiano kwani Ofisi yake iko wazi kupokea ushauri wenye lengo la kujenga nakuiletea maendeleo zaidi Wilaya hiyo.

Kessy alitumia nafasi hiyo pia kumshukuru Mhe. Rais Kwa kuendelea kuwaamini yeye na Mtangulizi wake Mohamed Hassan Moyo Kwa kuwapa nafasi Tena ya kuwa wakuu wa Wilaya akiitaja kuwa Imani waliyopewa ni deni Kwa Rais hivyo ni wajibu wao kumsaidia kikamilifu katika kufanikisha malengo ya Serikali katika kuwaletea maendeleo wanachi wake.

Kufuatia uteuzi wa Wakuu wa Wilaya wapya na mbadiliko ya Vituo vyankazi Kwa baadhi ya wakuu wa Wilaya, Mohamed Hassan Moyo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kwa Sasa amekuwa mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi na Veronica Kessy aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Kwa Sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: