Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angela Kairuki ameitaka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Kuharakisha zoezi la ulipaji fidia katika eneo linalohitajika kujengwa Sekondari Kata ya Kitunda Jimbo la Ukonga.


Kairuki Amesema hayo Leo Jijini Dar es Salaam katika ziara yake ya siku ya kwanza ambapo ametembelea Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

" Ninaomba fidia hii ilipwe ndani ya siku Saba hili taratibu za ujenzi wa shule uanze kuanza na muhakikishe mmefuata kanuni zote mthamini Mkuu wa Serikali hili kila upande upate Haki yake" Amesema Waziri Kairuki.

Waziri Kairuki Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dr Samia Suluhu Hassan imetenga fedha na ziko tayari hivyo Halmashauri harakisheni swala la fidia kwa kubali mlishapata na mmenileza hapa kuwa fedha za fidia ziko tayari hivyo nataka kuona ndani ya muda uliopangwa fedha zinalipwa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa amemshukuru Rais Dr Samia Suluhu kwa kuona Ilala na kuipatia fedha hizo ambazo zitakwenda kutatua Tatizo la elimu kwa wakazi hao wanaokaa pembezoni.

Mbunge huyo Amesema eneo la kitunda ni eneo ambalo watu wanahamia kwa wingi hivyo shule hiyo ni Muhimu kwa ajili ya Watoto.

Kwa upande kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,Tabu Shaibu amemueleza Waziri kuwa fedha hizo ziko tayari na kuanzia Jumatatu zitalipwa .

Amesema Halmashauri imepanga kumlipa mtu Mwenye eneo Hilo kiasi Cha Milioni 360.

Shule hiyo ambayo inajengwa kupitia fedha za mradi wa kuboresha elimu ya Sekondari Tanzania SEQIP.
Share To:

Post A Comment: