Na Denis Chambi, Tanga.
Kongamano la kutokomeza maadili potofu kwa watoto litakalohusisha madhehebu mbalimbali linataraiwa kufanyika jumamosi hii katika viwanja vya Pongwe jijini Tanga hii ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau wa maendeleo pamoja na serikali katika kupiga vita vitendo vya ukatili dhidi kwa watoto ndani ya jamii.
Kongamano hilo litaambatana pia na zoezi la upandaji wa miti katika viunga hivyo ikiwa ni kuhamasisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira ili kuepukana na athari mbalimbali ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza muandaaji wa kongamano hilo ambaye pia ni mchungaji wa kanisa la Tanzania Assembly of God 'TAG' mtoto wa simba wa kabila la Yuda na mwalimu wa mtoto mashuleni Agnes Willium alisema masuala ya malezi ya kiimani kana kwamba yametupiliwa mbali na jamii hivyo kupelekea janga la mmomonyoko wa maadili hasa kwa watoto wengi kufanyiwa vitendo vya ukatili jambo ambalo linakiuka taratibu na haki za kibinadamu huku viongozi wa dini nao wakihusishwa katika kutekeleza vitendo hivyo.
Alisema ni matarajio makubwa kama jamii inaweza kubadilika ikishirikiana kwa pamoja na juhudi za serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo huku akielekeza zaidi kuwalea waoto ambao ni taifa tegemezi la kesho kupitia malezi ya kiimani ambayo yatachangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa vitendo vya ukatili.
"Kongamano hili ni la dini zote na watu wote , Lengo kubwa ni kwaajili ya kutokomeza maadili potofu kwa watoto jamii ipate elimu kwa sababu wapo viongozi wa dini nao pia wanasababisha mmomonyoko wa maadili kutakuwa na maswala ya maadili, kujitambua kwa mtoto ili aweze kukabiliana na changamoto mbalimbali , na kufundisha kuhusu hofu ya Mungu ambayo ukiwa nayo huwezi kutenda dhambi sambamba na kupanda miti lakini kikubwa zaidi ni kutokomeza mmomonyoko aa maadili kwa watoto wetu hatimaye waweze kuwa na kizazi kizuri"
"Kuhusu kutokomeza ukatili wa watoto na wanawake tukiwa na maadili ya dini itasaidia sana lakini tuna maeneo matatu muhimu ambayo ni mzazi mwenyewe shuleni anakosoma pamoja na mafundisho ya dini akifundishwa vizuri anaweza kuwa mtu mzuri kabisa baadaye" alisema Mchungaji Agnes.
Post A Comment: