KATIBU Elimu Malezi na Mazingira wa Jumuiya ya Wazazi ya chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa akiongea na blog hii juu ya umuhimu wa kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.


Na Fredy Mgunda, Mufindi.

KATIBU Elimu Malezi na Mazingira wa Jumuiya ya Wazazi ya chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa amesema wamejipanga kuhakikisha wanatokomeza ukatilii wa kijinsia kwa watoto ili waweze kupata elimu bora.

Akizungumza na waandishi wa blog hii John Mgina ambaye ni Katibu Elimu Malezi na Mazingira wa Jumuiya ya Wazazi ya chama cha mapinduzi 'CCM) wilaya ya Mufindi alisema kuwa watoto wanahaki ya msingi ya kupata elimu bila kubaguliwa wala kufanyiwa ukatili wa kijinsia.

Mgina alisema kuwa kumekuwa na tabia kwa wazazi na walezi wa wilaya ya Mufindi kutowapeleka watoto shuleni kwa wakati na muda mwingine kuwanyima mahitaji muhimu yanayotakiwa shule.

Alisema kuwa kumfanyia ukatili wa kijinsia mtoto kutasababisha Taifa la Tanzania kutokuwa na wasomi wengi wa kuisaidia nchi kupiga hatua moja mbele ya kimaendeleo kama ilivyo kwa mataifa mengine.

Mgina alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi za ujenzi wa vyumba vya madarasa na kumaliza tatizo la uhaba wa madarasa hivyo wanafunzi wanatakiwa kwenda shule kusoma bila kikwazo chochote kile.

Alisema kuwa jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi hawatakubali kuona wanafunzi au Watoto wanafanyiwa ukatili wa kijinsia kwa namna yoyote ile hivyo wamejipanga kuanza kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wazazi ili kila mmoja ajue umuhimu wa Elimu kwa faida ya Taifa la Tanzania.

 Mgina alimazia kwa kuwataka wazazi wote Wilaya ya Mufindi kuwapeleka watoto wote shule kama yalivyo malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: