.

OR TAMISEMI

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza ujenzi wa wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Momba kukamilika kwa wakati kwa kuzingatia viwango na thamani ya fedha

Ameyasema hayo leo tarehe 14 Februari 2024 baada ya kukagua na kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya wilaya Momba mkoani Songwe.

Ujenzi wa Jengo hilo utagharimu shilingi bilioni 2.7 mpaka kukamilika ikihusisha na uwekaji wa samani za ndani ya jengo na ujenzi wa uzio.

Ujenzi wa awamu ya kwanza ulianza kutekelezwa tarehe 01/01/2022 na kukamilika tarehe 31/08/2022 kwa kutumia mkandarasi aitwaye Baren Enterprises. co. Ltd

Awamu ya pili ya Ujenzi wa Jengo hilo ilianza tarehe 01/01/2023 na inatarajia kukamilika 30/06/2023 chini ya Mhandisi Mshauri Wakala wa majengo Tanzania- TBA

Aidha, Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa Songwe kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa nyumba ya mkuu wa wilaya Momba ili aweze kuishi katika eneo lake la Kazi.

Waziri Mkuu amewataka Watumishi wa Halmashauri kuwajibika kikamilifu katika majukumu yao na kutatua kero za wannchi katika halmashauri ya wiaya Momba.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Mhe. David Silinde amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kusimamia kimamilifu ujenzi wa jengo hilo na miradi mingine ya maendeleo ili ikamilike na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Share To:

Post A Comment: